Loading...

Shehe Mkuu amuonya Mange Kimambi

Shehe Alhadi akizungumza na wanahabari katika mkutano huo
SHEHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa amemuonya mwanaharakati maarufu, Mange Kimambi kwa madai kuwa amemporomoshea matusi mazito baada ya kumuona mtandaoni amepiga picha na mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maulid Mtulya.

Shehe Alhadi ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa picha hiyo alipiga na mgombea huyo baada ya kukutana msibani ndipo baadhi ya wanachama wa CCM waliomba kupiga nae picha jambo ambalo asingeweza kulikataa alisema Alhadi.

Mange Kimambi
Alhadi akimkaribisha Mufti ofisini kwake na kisha kumshitakia ishu ya Mange Kimambi.

Aidha, Shehe huyo alisema hata kama alifanya makosa kupiga picha na mgombea huyo lakini hakustahili kutukanwa vile.

“Kama amezoea kuwatukana viongozi wa serikali asituchezee viongozi wa kidini, ulimi na mikono aliyopewa na Mwenyezi Mungu hakupewa kwa ajili ya kuwakashifu watu hivyo hapa alipochokoza sasa ameingia sipo, nasema mwaka huu hataumaliza salama.,” alisema Shehe Mussa.

Baada ya kusema hayo, Shehe Alhadi alimkaribisha, Mufti Abubakar Zuberi aliyemtembelea ofisini kwake akiwa kwenye ziara za kutembelea ofisi za Bakwata nchi nzima na kuwahimiza waislamu wote kuitambua na kuiunga mkono taasisi hiyo na kuepuka migogoro.
Shehe Mkuu amuonya Mange Kimambi Shehe Mkuu amuonya Mange Kimambi Reviewed by Zero Degree on 2/05/2018 05:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.