Mbowe 'amgeuzia kibao' Cyprian Musiba
Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe |
Mbowe amesema hayo leo Februari 27, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari kabla ya kwenda kuripoti Makao Makuu ya jeshi la polisi ambapo walikuwa wanakwenda kuripoti
Mbowe aliendelea kusema kuwa mtu huyo alitumwa kusema vile ili kuliandaa taifa juu ya kuja kukamatwa kwao kutokana na tukio lililotokea Februari 16, 2018 ambalo lilipelekea kifo cha mwanafunzi mmoja na watu wengine kujeruhiwa kwa kupigwa risasi, Mbowe anasema toka kutokea kwa tukio hilo kumekuwa na jitihada kubwa kuhakikisha viongozi hao wa CHADEMA wanahusishwa.
"Majuzi amejitokeza mtu anaitwa Musiba na akanishambulia kwamba CHADEMA na Mbowe ni watu hatari na viongozi wangu kadhaa wametajwa pamoja na viongozi wa vyama vingine na taasisi zingine, yule mtu akatoa shtuma za kipumbavu kabisaa, tena akizihusiha nchi ambazo ni washirika wetu wa maendeleo, yule bwana hakusema yeye yale maneno bali amelishwa yale maneno" alisema Mbowe.
Mbowe aliendelea kusema kuwa mtu huyo alitumwa kusema vile ili kuliandaa taifa juu ya kuja kukamatwa kwao kutokana na tukio lililotokea Februari 16, 2018 ambalo lilipelekea kifo cha mwanafunzi mmoja na watu wengine kujeruhiwa kwa kupigwa risasi, Mbowe anasema toka kutokea kwa tukio hilo kumekuwa na jitihada kubwa kuhakikisha viongozi hao wa CHADEMA wanahusishwa.
"Ili kuliandaaa taifa na mazingira ya kuwakamata kina Mbowe, Heche, mtu yule anasema tunafundisha vijana zaidi ya mia nne Ujerumani namna ya kuleta vurugu nchini na akaenda mbele zaidi na kusema kuwa kijana Yericko Nyerere. Yericko Nyerere hajawahi kufundishwa na chama hiki na wala hajawahi kuwa mtendaji wa chama hiki bali ni Mtanzania mwenye mapenzi mema na Demokrasia na mwanachama wetu"
"Sasa hawa wanaliandaa taifa na wanaandaaa katika style za kijinga ambazo zinafanya hata mahusiano yetu na mataifa makubwa nje yaingie kwenye doa na kuleta shida kwa mambo ambayo hayana maana hiyo yote ni katika kuuwa demokrasia katika nchi hii" alisisitiza Mbowe
Mbowe 'amgeuzia kibao' Cyprian Musiba
Reviewed by Zero Degree
on
2/27/2018 01:42:00 PM
Rating: