Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 27 Februari, 2018

Eden Hazard dhidi ya mabeki wa FC Barcelona
Chelsea itampa Eden Hazard ofa ya mkataba mpya wenye thamani ya karibu sawa na pauni 300,000 kwa wiki, pamoja na kwamba Real Madrid ina nia ya kumsajili.

Arsenal itafanya uamuzi juu ya nafasi ya Arsene Wenger kwenye majira ya joto - huku chaguo la peke likionekana kuwa ni kumaliza utawala wa miaka 22 wa Mfaransa huyo.

Orodha ya wanaotarajiwa kurithi nafasi ya Wenger ni pamoja na Mkufuzi wa Timu ya Taifa ya Ujerumani, Joachim Low, Mkufunzi wa Monaco, Leonardo Jardim, Mkufunzi Celtic, Brendan Rodgers na aliyekuwa kiungo wa klabu ya Arsenal, Mikel Arteta.

Kiungo wa klabu ya Lazio, Sergej Milinkovic-Savic amekiri kuwa amejisikia faraja sana baada ya Manchester United kuonyesha nia ya kutaka kumsajili lakini raia huyo wa Serbia anaonekana kufuahia maisha nchini Italia.

Manchester United imeungana na Real Madrid pamoja Barcelona kwenye mbio za kuwania saini ya beki wa klabu ya Real Sociedad, Alvaro Odriozola baada ya kutuma skauti akamchunguze nyota huyo wakati mechi ya klabu hiyo dhidi ya Red Bull Salzburg kwenye Europa Ligi Alhamisi iliyopita. (Daily Mail)

Klabu ya PSG imekanusha ripoti zinazodai kuwa mshambuliaji wao, Neymar Jr atafanyiwa upasuaji.

Timu ya Taifa ya Italia ina matamanio makubwa ya kumrejesha Antoni Conte kama mkufunzi mkuu wa kikosi chao.

Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema kuwa hana ndoto nyingine anzotaka kutimiza katika soka na anaweza kustaafu akiwa na furaha.

Winga wa klabu ya Swansea, Jefferson Montero amerejea Ecuador kwa mkopo katika klabu yake ya zamani, Emelec. (Sky Sports)

Chipikizi wa klabu ya Paris Saint-Germain, Yacine Adli anawindwa na Arsenal, Juventus pamoja na Barcelona.

Timu ya Taifa ya Ufaransa inaweza kumkosa winga wa klabu ya Bayern Munich, Kingsley Coman kwenye Kombe la Dunia katika kipindi cha majira ya joto baada ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 kufanyia upasuaji wa kifundo cha mguu. (L'Equipe)

Bayern Munich imejiunga na Manchester United pamoja na Liverpool kwenye mbio za kuwania saini ya winga wa klabu ya Sporting Lisbon, Gelson Martins.

Wakala wa Christian Eriksen amelifananisha suala la nyota huyo wa Tottenham kuhusihwa na uhamisho wa gharama kwenda Manchester United, Barcelona na Real Madrid kama heshima kubwa.

Nyota wa Timu ya Taifa ya Uhispania U21, Dani Ceballos ameiambia klabu ya Real Madrid kuwa antaka kujiunga na Liverpool.

Barcelona inatarajiwa kupeleka ofa kubwa mezani kumnasa beki wa klabu ya Tottenham, Toby Alderweireld ambaye amesusia kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo uya Uingereza.

Beki wa klabu ya Brighton, Ben White amekataa kusaini mkatana mpya katika klabu hiyo, huku Liverpool na Tottenham zikiwa na nia ya kumsajili. (Sun)

Meneja mpya wa klabu ya Borussia Dortmund anatarajiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Ujerumani mwezi April.

Max Meyer amekataa kusaini mkataba mpya na klabu ya Shalke 04, huku Arsenal ikiwa na nia ya kumsajili nyota huyo kwenye majira ya joto (Bild)

Carlo Ancelotti yuko tayari kuinoa klabu ya Arsenal kama Arsene Wenger atafukuzwa, huku Muitaliano huyo akiwaambia marafiki zake kuwa ana hamu sana ya kurejea katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Chelsea imezungumza na Luis Enrique pamoja na Thomas Tuchel kuhusu kuchukua nafasi ya Antonio Conte mwisho wa msimu huu.

Jose Mourinho amejipanga vilivyo kuhakikisha Pep Guardiola hampindui katika kumsajili nyota wa klabu ya Real Madrid, Isco kwenye majira ya joto.

Toby Alderweireld
Manchester United ina nafasi kubwa ya kufanikisha usajili wa beki wa klabu ya Tottenham, Toby Alderweireld kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo, Daniel Levy.

Gareth Bale ameshtukia mipango ya Real Madrid kutaka kumtumia katika dili la kubadilishana na klabu ya Liverpool kwa lengo la kumpata Mohamed Salah kwenye majira ya joto. (Star)

Yannick Carrasco amekanusha taarifa zinazodai kuwa ameondoka Atletico Madrid kwenda Dalian Yifang ya China kwa sababu ya fedha, akidai kuwa bado anataka kupata nafasi kwenye kikosi cha Ubelgiji kitakachoshiriki Kombe la Dunia kwenye majira ya joto. (Marca)

Shirikisho la soka litapanga michuano ya FA Cup ya raundi ya tano kuchezwa katikati ya wiki kupihsa Mapumziko ya Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu wa baridi mwezi Februari kuanzia msimu wa 2019/20.

Newcastle iko katika shinikizo kubwa la kufukuza kazi Peter Beardsley baada ya kupokea malalamiko makubwa ya kiubaguzi yanayomkabili mkufunzi huyo wa kikosi chao cha wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 23. (Times)

Manchester City wameruhisiwa kumsajili kwa mara nyingine tena kinda ambaye alisababisha wafungiwa baada ya kumsajili akiwa na miaka 11.

Tottenham iko tayari kulipa kiasi cha pauni milioni 35 kunamsa chipukizi wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon kwenye majira ya joto. (Telegraph)

Waendesha mashtaka wa La Liga wanataka kiungo wa Manchester United, Ander Herrera afungwe miaka minne kwa kosa la kupanga matokeo.

West Ham watarejea sokoni kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Anderlecht, Leander Dendoncker kwenye majira ya joto wakati Fiorentina wakifikiria kutoa ofa ya kumnasa kiungo wa wagonga nyundo, Pedro Obiang.

Aliyekuwa nyota wa klabu ya West Ham, Dimitri Payet alitishia kumuumiza Neymar kabla mshambuliaji huyo wa PSG hajapata majera katika kifundo cha mguu katika mechi yao dhidi ya Marseille.

Southampton inatarajiwa kuungana na Newcastle kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Marseille, Andre-Frank Zambo Anguissa. (Mirror)

Arsenal wameanzisha mkakati wa kumsajli kiungo wa klabu ya Nice, Jean Michael Seri lakini wanakabiliana na ushindani kutoka Manchester United na Liverpool.

Aliyekuwa kiungo wa Real Madrid na Kocha wa sasa wa timu yao ya U19, Guti 
Real Madrid wataachana na mpango wa kumsajili David De Gea kama Guti atachukua nafasi ya Zinedine Zidane kama meneja mkuu mwisho wa msimu huu.

Southampton wanajiandaa kujaribu kumsajili mshmbuliaji wa Ostersunds, Saman Ghoddos, ambaye alitengeneza magoli yao yote ya Europa Ligi dhidi ya Arsenal wiki iliyopita. (Express)

Kwa mujibu wa Ray Parlour, aliyekuwa kiungo wa klabu ya Arsenal na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Patrick Viera anaweza kuwa mtu sahihi anayefaa kuchukua nafasi ya Arsene Wenger. (talkSport
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 27 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 27 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/27/2018 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.