Loading...

Mexico: Timu ya soka yakataa kubeba bendera ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya


Wachezaji kutoka timu ya mpira wa miguu nchini Mexico, Pumas walikataa ombi la kubeba bendera za kundi linalopigana vita kupambana na madawa ya kulevya kabla ya mechi wikendi iliyopita.

Maskani ya timu ya Pumas yako karibu na Chuo Kikuu cha National Autonomous University, maarufu kama UNAM.

Raia wawili waliuawa kwa kupigwa risasi katika mazingira ya chuo hicho wiki iliyopita na waendesha mashtaka wanasema mauaji hayo inaonekana kuwa ni sehemu ya migogoro inayowahusisha wauzaji wa madawa ya kulevya ambao wanafanya biashara hiyo hadahrani katika chuo hicho.

Mkuu wa chuo hicho, Enrique Graue alikiambia chombo kimoja cha habari nchini humo kwamba, viongozi wa chuo waliwaomba wachezaji wa Pumas wabebe bendera zilioandikwa “Narcos out of the UNAM” katika mechi yao dhidi ya Chivas siku ya Jumapili.

Kwa mujibu wa Gazeti la michezo la Record, wachezaji kadhaa waligoma kufanya hivyo kwa hofu ya usalama wao na badala yake, chuo hicho kiliweka ujumbe huo kwenye ubao wa matokeo.
Mexico: Timu ya soka yakataa kubeba bendera ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya Mexico: Timu ya soka yakataa kubeba bendera ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya Reviewed by Zero Degree on 2/28/2018 11:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.