Loading...

Orodha ya nchi zote zitakazotembelewa na Kombe la Dunia

Ni rais huyo pekee aliyeruhusiwa kuligusa kombehilo nchini Kenya. Kando na marais, ni wachezaji waliowahi kushinda kombe hilo pekee ambao huruhusiwa kuligusa
Wakenya wamejitokeza kwa wingi kulitazama na kupigwa picha na Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) ambalo limekuwa nchini humo kwa siku mbili.

Kombe hilo ambalo liliwasili nchini Kenya na kupokelewa na Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta lilipata watazamaji wengi ambao walifika kujionea na kupiga picha pamoja na kombe hilo.

Raia wa kawaida hawakuruhusiwa kuligusa kombe hilo, na badala yake walilitazama likiwa katika sanduku la Kioo.

Kombe hilo linatembezwa mataifa mbalimbali kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza Juni, nchini Urusi. Na ni mara ya tatu kwa kombe hilo kuwa nchini Kenya, awali ikiwa 2010 na 2013 katika ya fainali zilizofanyika Afrika Kusini na Brazil.

Kabla ya kutua Kenya, kombe hilo lilikuwa nchini Sudan kisha Ethiopia.

Hata hivyo ziara ya kombe hilo bado inaendelea ambapo limeondoka nchi Kenya na kuelekea Maputo, Msumbiji.

Nchi nyingine za Afrika zinazotarajia kufikiwa na ziara hiyo ya Kombe la Dunia ni Afrika Kusini, Uganda, Nigeria, Senegal, Cote D’Ivoire (Ivory Coast) kisha Misri.

Baada ya ziara ya kombe hilo barani Afrika kukamilika, litaelekea barani Ulaya kuendelea na ziara yake kabla ya kuanza mchuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Urusi, Juni 14, mwaka huu.

Hapa chini ni ratiba nzima ya ziara ya Kombe la Dunia katika nchi mbalimbali duniani. Zipo nchi ambazo tayari zimeshatembelewa na nyingine zinaendelea kutembelewa (Mpangilio uko hivi: Jina la Kituo, Nchi na Tarehe).
  • Colombo, Sri Lanka, Tarehe 23 - 24 January
  • Male, Maldives, Tarehe 24-25 January
  • Phuket, Thailand, Tarehe 26-27 January
  • Vientiane, Laos, Tarehe 28 January
  • Macau, China P.R, Tarehe 29 January
  • Nukualofa, Tonga, Tarehe 31 January
  • Honiara, Solomon Islands, Tarehe 1 February
  • Port Moresby, Papua New Guinea, Tarehe 2 February
  • Lahore, Pakistan, Tarehe 3 February
  • Almaty, Kazakhstan, Tarehe 4 February
  • Bishkek, Kyrgyz Republic, Tarehe 5 February
  • Dushanbe, Tajikistan, Tarehe 5 February
  • Tashkent, Uzbekistan, Tarehe 6 February
  • Ashgabat, Turkmenistan 7 February
  • Yerevan, Armenia, Tarehe 7 February
  • Tblisi, Georgia, Tarehe 8 February
  • Baku, Azerbaijan, Tarehe 9 February
  • Valetta, Malta, Tarehe 10 February
  • Vienna, Austria, Tarehe 11 February
  • Minsk, Belarus, Tarehe 13 February
  • Sofia, Bulgaria, Tarehe 14 February
  • Tel Aviv, Israel, Tarehe 15 February
  • Larnaca, Cyprus, Tarehe 16 February
  • Ramallah, Palestine, Tarehe 17-19 February
  • Amman, Jordan, Tarehe 20 February
  • Dubai, United Arab Emirates, Tarehe 21 February
  • Khartoum, Sudan, Tarehe 22-23 February
  • Addis Ababa, Ethiopia, Tarehe 24-25 February
  • Nairobi, Kenya, Tarehe 26-27 February
  • Maputo, Msumbiji, Tarehe 28 February
  • Johannesburg, Afrika Kusini, Tarehe 1-2 March
  • Cape Town, Afrika Kusini, Tarehe 3 March
  • Kampala, Uganda, Tarehe 5-6 March
  • Abuja, Nigeria, Tarehe 7-8 March
  • Lagos, Nigeria, Tarehe 9-10 March
  • Dakar, Senegal, Tarehe 11-12 March
  • Abidjan, Cote d’Ivoire, Tarehe 13-14 March
  • Cairo, Misri, Tarehe 15-16 March
  • Naples, Italy, Tarehe 17-19 March
  • Paris, France, Tarehe 20-21 March
  • Cologne, Germany, Tarehe 22-23 March
  • Oslo, Norway, Tarehe 24 March
  • Torshavn, Faroe Islands, Tarehe 24-25 March
  • Reykjavik, Iceland, Tarehe 25 March
  • Tucuman, Argentina, Tarehe 27-28 March
  • Berazategui, Argentina, Tarehe 29 March
  • Buenos Aires, Argentina, Tarehe 30-31 March
  • Rosario, Argentina, Tarehe 1-2 April
  • Bogota, Colombia, Tarehe 3-5 April
  • Panama City, Panama, Tarehe 6 April
  • San Jose, Costa Rica, Tarehe 7-8 April
  • Guadalajara, Mexico, Tarehe 9-10 April
  • Monterrey, Mexico, Tarehe 11-12 April
  • Mexico City, Mexico, Tarehe 13-15 April
  • New York, USA, Tarehe 16 April
  • Miami, USA, Tarehe 17 April
  • Los Angeles, USA, Tarehe 18-20 April
  • Frankfurt, Germany, Tarehe 22 April
  • Ulaanbaatar, Mongolia, Tarehe 23 April
  • Beijing, China P.R, Tarehe 25 April
  • Shanghai, China, Tarehe P.R 26 April
  • Tokyo, Japan, Tarehe 27-28 April
  • Osaka, Japan, Tarehe 29-30 April
  • Vladivostok, Russia, Tarehe 1 May
Orodha ya nchi zote zitakazotembelewa na Kombe la Dunia Orodha ya nchi zote zitakazotembelewa na Kombe la Dunia Reviewed by Zero Degree on 2/28/2018 12:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.