Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 28 Februari, 2018

Harry Kane na meneja wake, Mauricio Pochettino
''Tottenham itaweza kukataa ofa ya pauni milioni 200 kwa ajili ya uhamisho wa Harry Kane?'' - David Ginola. (talkSport)

Beki wa klabu ya Brighton, Gaetan Bong amesaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaoisha mwaka 2019.

Mkufunzi wa Timu ya Taifa ya Wales, Ryan Giggs anasisitiza kuwa Gareth Bale anafurahia kuwa Real Madrid, licha ya kuwepo kwa tetesi zinazomhusisha na uhamisho kwenda Ligi Kuu ya Uingereza.

Arsene Wenger anasema kuwa hahofii nafasi yake ya kazi na badala yake yuko makini na mechi ijayo dhidi ya Manchester City Alhamisi. (Sky Sports)

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham, Daniel Levy anasema kuwa klabu hiyo ya haitauza wachezaji ambao meneja wao, Mauricio Pochettino anawahitaji.

Kiungo wa klabu ya Roma, Radja Nainggolan anasema kuwa aliachana na ofa ya kujiunga Chelsea ili abaki nchini Italia. (ESPN)

Manchester United hawana uhakika wa kumbakisha Marouane Fellaini, ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu huu.

West Brom itamkosa Daniel Sturridge, ambaye alisajiliwa kwa mkopo kutoka Liverpool kwa sababu ya majeraha katika paja.

Alan Pardew ameiambia West Brom kuwa anataka kuendelea kuinoa klabu hiyo na kujaribu kuirejesha Ligi Kuu kama itashuka daraja.

Beki ya Manchester City itaigharimu klabu hiyo kukosa nafasi ya kutwaa taji la Ulaya, kwa mujibu wa Louis van Gaal.

Joe Allen
Stoke City itakabiliana na ushindani kumbakisha kiuno wa Timu ya Taifa ya Wales, Joe Allen klabu hiyo itashuka daraja.

Bournemouth inatazamia kumsajili kiungo wa klabu ya Lokomotiv Moscow, Anton Miranchuk kama mtu sahihi anayefaa kuchukua nafasi ya Harry Arter, ambaye anatarajiwa kuondoka kwenye majira ya joto. (Mirror)

Jose Mourinho hafurahii kitendo cha klabu ya Manchester United kuchelewesha mikataba mipya ya wachezaji.

Meneja wa Timu ya Taifa ya Wales, Ryan Giggs anataka kuona Aaron Ramsey anakamilisha masuala yake, huku kiungo huyo wa Arsenal akikaribia kumaliza mkataba wake. (Daily Mail)

Matumaini ya Luis Enrique kurithi nafasi ya Antonio Conte katika klabu ya Chelsea yatategemeana na kama atakuwa tayari kukubali mshahara mdogo kuliko aliokuwa analipwa Barcelona.

Alex McLeish anatarajia kufanya mazungumzo na Scott McTominay katika uwanja wa mazoezi wa klabu ya Manchester United wiki hii ili kujaribu kumshawishi nyota huyo aahidi kuichezea Timu ya Taifa ya Uskoti.

Farhad Moshiri, ambaye ana sehemu kubwa ya hisa za klabu ya Everton, lazima aamue kama atabaki na Sam Allardyce msimu ujao au la. (Telegraph)

Juventus imetoa siku saba kwa kiungo wa klabu ya Liverpool, Emre Can kukubaliana na vigezo alivyopewa na vigogo hao wa Serie A.

Everton iko kwenye mchakato wa kumsaka mtu sahihi anayefaa kuchukua nafasi ya Sam Allardyce kwenye majira ya joto.

Kibarua cha Antonio Conte kama meneja wa klabu ya Chelsea kiko salama kwa sasa kwa sababu Luis Enrique hahitaji kuchukua kibarua hicho hadi mwisho wa msimu.

Ripoti zinadai kuwa Max Meyer amekataa kusaini mkataba mpya katika klabu ya Schalke, na kuzichochea Liverpool na Arsenal kwenye mbio za kuwania saini yake kwenye majira ya joto.

Jorginho
Liverpool wanaiongoza Juventus katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa Napoli, Jorginho. (Star)

Real Madrid imegeukia kwa mshambuliaji anayewindwa na Chelsea pamoja na Manchester United, Robert Lewandowski baada ya Spurs kukataa ofa yao ya kumnasa Harry Kane.

Antonio Conte atapewa ofa ya kurejea katika kibarua cha kuinoa Timu ya Taifa ya Italia kabla msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza haujaisha.

Phil Foden atapewa ofa ya mkataba mpya wenye maslahi mazuri atakapofikisha umri wa miaka 18 Tarehe 28,mwezi Mie. (Sun)

Meneja wa klabu ya Monaco, Leonardo Jardim anataka kuchukua nafasi ya Arsene Wenger, endapo Arsenal itaamua kufanya mabadiliko kwenye majira ya joto.

Benchi la ufundi la Uingereza limemfanyia uchunguzi chipukizi wa Fulham, Ryan Sessegnon katika zaidi ya mechi moja msimu huu lakini anabaki kuwa na nafasi ndogo kwenye kikosi cha Kombe la Dunia. (Independent)

Ripoti zinadai kuwa Liverpool iko tayari kumoa Mohamed Salah ofa ya mkataba mpya na raia huyo wa Misri atasaini kwa furaha.

Real Madrid wako tayari kumuuza kiungo wa klabu hiyo, Dani Ceballos kwenda Liverpool kwenye majira ya joto.

Inadaiwa Lionel Messi hafurahii kitendo cha klabu ya Barcelona kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann. (Express)

Gareth Southgate na Rashford
Gareth Southgate anazidi kuwa na wasiwasi juu Marcus Rashford kukosa muda wa kutosha katika kikosi cha Manchester United kuelekea michuano ya Kombe la Dunia kwenye majira ya joto. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 28 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 28 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/28/2018 01:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.