Loading...

Mkutano wa wakuu wa EAC waanza Uganda


MKUTANO wa 19 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umeanza Munyonyo jijini Kampala, Uganda.

Marais wa nchi kadhaa wanachama EAC tayari wapo ukumbini akiwemo Rais wa Tanzania, John Magufuli, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, na mwenyeji wao Rais Yoweri Museveni.

Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Liberat Mfumukeko amesema, mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kujadili masuala ya miundombinu ndani ya nchi sita za EAC, afya na maendeleo kwa ujumla.

Nchi wanachama wa EAC ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini. Kwa mujibu wa taarifa ya Sekretarieti ya EAC kwa umma, mkutano huo unatarajiwa kushirikisha wajumbe zaidi ya 1,000 wa ndani na nje ya nchi wanachama wa jumuiya.

Wakuu wa nchi wanatarajiwa kujadili masuala ya miundombinu, fedha za tiba na maendeleo kwa kutumia kaulimbiu ‘Kukuza na kapanua mtangamano kwenye miundombinu na maendeleo ya sekta ya afya kwenye nchi wanachama EAC’.

Mkutano wa Kampala umeandaliwa na sekretarieti ya EAC kwa kushirikiana na nchi wanachama wa jumuiya hiyo, na wadau wakubwa wa maendeleo kwenye eneo hilo.

Utakuwa mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi za EAC kuzungumzia masuala ya afya na utakuwa wa nne kuhusu kugharamia miundombinu na maendeleo.

Mkuu wa Mawasiliano kwenye Sekretarieti ya EAC, Richard Owora Othieno kupitia taarifa yake amesema wakuu wa nchi wanatarajiwa kuzungumzia maendeleo ya miradi ikiwemo miundombinu bora, ya uhakika, endelevu, imara na inayotolewa haraka ikiwemo wa kieneo na ile ya kuvuka mipaka ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi na hali bora za mwananchi.
Mkutano wa wakuu wa EAC waanza Uganda Mkutano wa wakuu wa EAC waanza Uganda Reviewed by Zero Degree on 2/22/2018 12:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.