Rais wa FIFA, Gianni Infantino atua nchini
Gianni Infantino akilakiwa na Waziri Mwakyembe na Rais wa TFF, Wallace Karia katika Uwanja wa Ndege JNIA, Dar |
Infantino akiongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Ahmad Ahmad walipokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe walioongozana na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Rashid Ali Juma na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar.
Rais huyo wa FIFA akiwa uwanjani hapo baada ya kuwasili alipata fursa ya kuzungumza na waziri Mwakyembe ambapo alimtaja nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, anayecheza soka la kulipwa KRC Genk ya Ubelgiji.
Mbwana Samatta akiitumikia Genk |
“Nilisikia mchezaji bora wa Afrika kutoka Tanzania, Mbwana Samatta, anayecheza Genk, hii ni nchi ya mpira licha ya changamoto za shirikisho siku za nyuma, lakini kwa sasa mpo kwenye mstari kutokana na uongozi mpya kwa kushirikiana na CAF na FIFA,” alisema Infantino.
Rais wa FIFA, Gianni Infantino atua nchini
Reviewed by Zero Degree
on
2/22/2018 11:15:00 AM
Rating: