Loading...

Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia

Rais Magufuli alipokwenda kummjulia hali Mzee Kingunge hospitalini
Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia ya alfajiri leo Ijumaa Februari 2,2018 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.

Mke wa Kingunge Peras Ngombalemwiru alifariki dunia mwanzoni mwa mwezi January kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo.

Mzee Kingunge alikuwa kiongozi mwandamizi nchini Tanzania katika serikali za awamu nne zilizopita na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali zikiwemo ukuu wa mikoa ya Tanga na Singida, Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi na Waziri katika wizara mbalimbali
Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia Reviewed by Zero Degree on 2/02/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.