Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 2 Februari, 2018

Kiungo wa klabu ya Leicester City na timu ya taifa ya Algeria, Riyad Mahrez
Gus Poyet ameikosoa klabu ya Leicester City kwa kitendo cha kumzuia Riyad Mahrez kwenda Manchester City.

Edin Dzeko amesema kuwa kitendo cha klabu ya Chelsea kuonyesha nia ya kutaka kumsajili ni heshima kwake.

Klabu ya Arsenal inafikiria kumsajili golikipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak achukue nafasi ya Petr Cech kwenye majira ya joto.  

Meneja wa klabu ya Southampton, Maurcio Pellegrino amesema kuwa klabu yake ilishindwa kuongeza nguvu mpya kikosini kwa sababu ya bei kubwa za wachezaji katika soko la usajili. (talkSport)

Meneja wa Manchester United amekanusha taarifa zinazodai kuwa Zlatan Ibrahimovic anatarajia kuondoka kwenda LA Galaxy.

Meneja wa Leceister City ana matumain kwamba Mahrez ataweka kando mambo yote yaliyopita na kurejea mazoezini.

Meneja wa Burnley, Sean Dyche alisema kuwa kiungo wa klabu hiyo, Steven Defour anatarajia kufanyiwa upauaji wa goti.

Pep Guardiola amesema kuwa vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza bado haijaisha.

Conte amekanusha kufanya mazungumzo shirikisho la soka la Italia kuhusu kibarua cha kuionoa timu ya taifa hilo. (Sky Sports)


Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anaamini kwamba pesa iko inaharibu mchezo wa mpira wa miguu. (ESPN)

Pierre-Emerick Aubameyang ataivaa jezi namba 14 kwa kipindi cha msimu kilichosalia kama mchezaji wa Arsenal na ana matumaini ya kuichukua jezi namba 17 inayotumiwa na Alex Iwobi 17 katika msimu wa 2018-19.

Chelsea ina matumaini kwamba mvutano uliokuwepo kati ya klabu na meneja Antonio Conte utaisha kufuatia kufungwa kwa dirisha la usajili, huku klabu hiyo ikitarajia mafanikio. (Mirror)

Kiungo wa Manchester United, Marouane Fellaini atakua nje kwa muda wa miezi miwili kufuatia majeraha ya goti aliyopata kwenye mechi dhidi ya Tottenham.

Nahoda wa Manchester City, Vincent Kompany anafikiria kuhusu nafasi yake katika kikosi cha timu yake ya taifa ya Ubelgiji kwa lengo la kuendelea na kazi yake katika klabu hiyo ya Uingereza.

Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) bado linafanya uchunguzi juu ya kitendo cha kibaguzi ambacho Mason Holgate wa Everton anadai alifanyiwa na straika wa Liverpool, Roberto Firmino. (Telegraph)

Jose Mourinho alikasirishwa na kiwango cha Anthony Martial kwenye mchezo wao dhidi ya Tottenham.

Real Madrid inatarajiwa kumrejesha James Rodriguez kutoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu wake wa kwanza nchini Ujerumani. (Express)

Manchester United ina uhakika wa kufanikisha uhamisho wa beki wa klabu ya Barcelona, Samuel Umtiti kwenye majira joto. (Star)

Timu ya taifa ya Italia iko tayari kumpa ofa Antonio Conte ya kuondoka katika klabu ya Chelsea kwa urahisi.

Leicester iligoma kumruhusu Islam Slimani ajiunge na klabu ya West Ham kwa mkopo baada ya maoni ya Karren Brady juu ya kufukuzwa kwa Claudio Ranieri msimu uliopita.

Wachezaji wa Leicester wamemgeuka Riyad Mahrez baada ya kukosa mazoezini siku ya Alhamisi.

Klabu ya Roma inasema haikuweza kumudu uhamisho wa beki wa Manchester Uinted, Daley Blind mwezi Januari.

Diego Maradona
Wakala wa Diego Maradona anadai raia huyo wa Argentina alizuiwa kuingia nchin Marekani baada ya kutoa maoni kuhusu mienendo ya rais wa taifa hilo, Donald Trump.

Chris Coleman amehoji juu ya utayari wa Jack Rodwell kujitoa kwa klabu yaek baada ya kiungo huyo kukataa Sunderland. (Sun)

Arsene Wenger yuko tayari kumwanzisha Aubameyang kwenye mchezo wao dhidi ya klabu ya Everton siku ya Jumamosi licha ya kwamba nyota huyo anasumbuliwa na homa.

Mmiliki wa klabu ya, Owen Oyston anajikuta katika kesi nyingine mahakamani baada ya kushindwa kumlipa pauni milioni 10 aliyekuwa mkurugenzi wa klabu hiyo, Valeri Belokon katika siku ya mwisho iliyopangwa. (Daily Mail)

Malalamiko ya Antonio Conte juu ya sera ya usajili katika klabu ya Chelsea yalianza baada ya klabu hiyo kushindwa kukamilisha uhamisho wa Alexis Sanchez, Alex Sandro na Virgil van Dijk kwenye majira ya joto. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 2 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 2 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/02/2018 08:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.