Loading...

Nassari apandishwa kizimbani


Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kujibu shtaka la shambulio.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Fortunatus Muhalila mbele ya hakimu Jasmine Abdul amedai kuwa Desemba 14,2014 Nassari alimshambulia aliyekuwa Mtendaji wa Kata ya Makiba, Neeman Ngudu.

Anadaiwa kutenda kosa hilo eneo la Makiba kwa kumpiga mateke Ngudu na kumsababishia maumivu akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Mwendesha Mashtaka Muhalila amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na ameiomba Mahakama kupanga siku nyingine ya kutajwa shtaka hilo.

Hata hivyo Mbunge huyo amekana kutenda kosa hilo.

Hakimu wa Mahakama hiyo ameahirisha kesi hadi Machi 6,2018 itakapotajwa na Mbunge huyo ameachiwa kwa dhamana ya bondi ya milioni tano iliyosainiwa na diwani Gabriel Mwanda wa Kata ya Ambuseri
Nassari apandishwa kizimbani Nassari apandishwa kizimbani Reviewed by Zero Degree on 2/06/2018 02:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.