Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 6 Februari, 2018

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte
Meneja wa Chelsea, Antonio Conte anafikiria kuwapa wachezaji wake siku tatu za mapumziko baada ya kufungwa goli 4-1 na Watford, ikiwa ni jaribio la kumaliza uchovu uliochangia majeruhi na utendaji mbovu.


Kwa mujibu wa Ahmed Hossam 'Mido', Mohamed Salah anaweza kufikisha magoli 100 katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Beki wa klabu ya Real Madrid ataikosa mechi ya PSG kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA).

Manchester United, Liverpool na Bayern Munich zinawania saini ya winga wa klabu ya Borussia Doetmund, Christian Pulisic.

Vincent Kompany bado yuko kwenye mipango ya meneja wa Manchester City, Pep Guardiola.

Antonio Conte amesema hana hofu ya kufukuzwa licha ya klabu yake kupata matokeo mabaya hivi karibuni, ambayo yanamweka katika hatari kubwa ya kutimuliwa. (ESPN)

Ripoti zinadai kuwa David Moyes anatarajia kuondoka West Ham mwishoni mwa msimu huu. 

Klabu ya Arsenal imeanza mazunguzo  na Aaron Ramsey juu ya mkataba mpya.

Karim Benzema
Manchester United na Arsenal zimepewa ofa ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Karim Benzema.

Aliyekuwa nyota wa klabu ya Chelsea na meneja, Ray Wilkins anasema kwamba wachezaji ndio waliomwangusha Antonio Conte. (talkSport)

Manchester City inafanya mpango wa kurejesha mashambulizi kwa kiungo wa  Leicester, Riyad Mahrez kwenye majira ya joto.

Alexis Sanchez anaanza mpango binafsi wa kujiweka fiti aendana na kasi katika klabu ya Manchester Utd. (Sun)

Kiungo wa klabu ya West Ham, Pedro Obiang amefanyiwa upasuaji wa goti.

Wayne Rooney amesema kuwa ana mpango wa kuingia kwenye kazi ya umeneja baada ya kustafu kucheza soka.

Klabu ya Leeds imemteua Paul Heckingbottom kuwa meneja mpya na kumpa mkataba wa mwaka mmoja na nusu. (Sky Sports)

Beki wa kulia anayewindwa na klabu ya Liverpool, Sime Vrsaljko amesaini mkataba mpya Atletico Madrid.

Mathieu Debuchy anadai Arsene Wenger alitibua dili lake la uhamisho kwenda Manchester United.

Alvaro Morata
Ripoti zinadai kuwa mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaowindwa na klabu ya PSG kwenye majira ya joto.

Arsenal inatarajia kuwa na mazungumzo magumu na Aaron Ramsey juu ya mkataba mpya.

Vincent Kompany amesema uwezekano wa kuondoka Manchester City kwenye majira ya joto ni mkubwa sana. (Mirror)

Wilfried Zaha anatarajiwa kuwa nje kwa miezi kadhaa na ataonana mtaalamu Jumanne ya leo.

Beki wa klabu ya Liverpool, Virgil van Dijk anasema anaweza kukabiliana na presha anayoipata kutokana na bei yake ya pauni milioni 75. (Guardian)

Newcastle itarejea sokoni kutafuta saini ya mshambukiaji wa Feyenoord, Nicolai Jorgensen kwenye majira ya joto. (Star)

Chelsea imefanya mazungumzo na klabu ya Real Madrid juu ya dili la kubadilishina Eden Hazard kwa Karim Benzema.

Troy Deeney anaweza kutiwa hatiani baada ya kushangilia goli lilofungwa na timu yake dhidi ya Chelsea kwa kuonyesha ishara ya kidole cha kati.

Wilson Tilve, 16
Manchester United imetoa wiki moja ya majaribio kwa chipukizi wa Colombia, Wilson Tilve.

Mmoja wa wamiliki wa klabu ya West Ham, David Sullivan anasema kuwa nyimbo za mashabiki zinazoshinikiza kuvunjwa kwa bodi ya klabu hiyo hazitasaidia chochote. (Daily Mail)

Ligi Kuu inaweza kuanzisha mapumziko mafupi kwenye majira ya baridi kabla ya mwaka 2022 ili kuifanya ligi hiyo iendane na ligi nyingine za Ulaya. (Times)


Uwezekano wa David Moyes kuendelea kukinoa kikosi cha West Ham msimu ujao ni mdogo sana.


Golikipa wa Arsenal, Petr Cech anatarajiwa kuikosa dabi ya kaskazini mwa London dhidi ya Tottenham kwa sababu ya majeraha. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 6 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 6 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/06/2018 12:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.