Petit: Muda wa Lacazette katika klabu ya Arsenal umekwisha
Mshambuluaji huyo aliyejiunga na washika bunduki kwenye majira ya joto mwaka jana kwa pauni milioni 53, amefunga goli moja tu katika mechi 12 zilizopita.
Klabu ya Arsenal itasafiri kwenda Wembley siku ya Jumamosi kucheza dhidi ya Tottenham.
Kuwasili kwa Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund kwa pauni milioni 56, kunaonyesha kuwa ni dhahiri Lacazette atakua chaguo la pili la klabu hiyo.
Aubameyang |
Aubameyang alifunga goli moja katika mechi yake ya kwanza akiwa Arsenal, ambapo klabu hiyo ya London iliibuka na ushindi wa goli 5-1 dhidi ya Everton, wakati Lacazette akiwa benchi.
Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Arsenal, Emmanuel Petit anasisitiza kuwa muda wa nyota huyo mwenye miaka 26 katika klabu hiyo uko ukingoni.
Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Arsenal, Emmanuel Petit anasisitiza kuwa muda wa nyota huyo mwenye miaka 26 katika klabu hiyo uko ukingoni.
Emmanuel Petit |
Akizungumza na 'The Sun', Petit alisema ''Lacazette yuko katika msukumo mkubwa. Anatakiwa kubadilika au akubali kundoka kwenye majira ya joto.
''Kuwasili kwa Aubameyang ni jibu tosha kwangu kwamba, inawezekana tayari muda umeshakwisha na imani ya Arsene Wenger kwa Lacazette imeisha.''
''Baada ya miezi sita katika klabu hajaonyehsa uwezo mkubwa, hivyo Aubameyang ni mtu sahihi ambaye Arsenal inamhitaji.''
Klabu ya Arsenal itasafiri kwenda Wembley siku ya Jumamosi kucheza dhidi ya Tottenham.
Petit: Muda wa Lacazette katika klabu ya Arsenal umekwisha
Reviewed by Zero Degree
on
2/09/2018 05:00:00 PM
Rating: