Loading...

Serikali kulipa madeni ya walimu mwezi huu


Waziri wa fedha na Mipango Dr.Philip Mpango amesema Serikali italipa madeni inayodaiwa ya Zaidi ya shilingi bilioni 43 ambazo imezihakiki na kuona kuwa ni madeni halali ambayo wanadaiwa kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2017 na watumishi wa umma wakiwemo Walimu.

Waziri Mpango amesema fedha hizo zitalipwa kwa mkupuo na watumishi watakaolipwa madai hayo ni elfu ishirini na saba mia tatu themanini na tisa na yatalipwa sambamba na mishahara ya mwezi huu wa pili.

Waziri Mpango amesema awali watumishi elfu themanini na mbili mia moja kumi na moja waliwasilisha madai ya shilingi bilioni mia moja na ishirini na saba, milioni mia sita na tano laki moja na ishirini na nane, mia nane na sabini na mbili na senti themanini na moja. 

Kwa mujibu wa Waziri Mpango,Serikaki imeokoa shilingi bilioni themanini na nne na milioni mia mbili na laki mbili kufuatia uhakiki huo ambazo ni sawa na asilimia 66 ya madai yote yaliyokuwa yamewasilishwa awali.
Serikali kulipa madeni ya walimu mwezi huu Serikali kulipa madeni ya walimu mwezi huu Reviewed by Zero Degree on 2/09/2018 04:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.