Loading...

Polisi wavamia Mkutano wa Zitto Kabwe

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe
Mkutano wa ndani wa Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe uliokuwa unafanyika katika Kata ya Nambisi, wilayani Mbulu umevamiwa na Polisi wakiwa katika magari ya Defender.

Taarifa iliyotolewa leo na Afisa Habari wa Chama hicho, imeeleza kuwa polisi baada ya kuzungumza na Mwenyekiti wa Mkoa Manyara na kuelezwa kuwa kikao ni cha ndani hakihitaji taarifa Polisi wameondoka na kuagiza diwani wa kata huyo kuripoti kituo cha Polisi.

Taarifa kwa waandishi:
MKUTANO wa ndani wa Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe uliokuwa unafanyika katika Kata ya Nambisi, wilayani Mbulu umevamiwa na Polisi wakiwa katika magari ya defender.

Baada ya kuzungumza na Mwenyekiti wa Mkoa Manyara na kuelezwa kuwa kikao ni cha ndani hakihitaji Taarifa Polisi wameondoka na kuagiza diwani Wa kata huyo kuripoti kituo cha Polisi.


Abdallah Khamis
Afisa Habari
ACT Wazalendo
26/02/2018

Zitto yupo katika ziara ya mikoa 8 kutembelea Kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua Madiwani kutoka chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Polisi wavamia Mkutano wa Zitto Kabwe Polisi wavamia Mkutano wa Zitto Kabwe Reviewed by Zero Degree on 2/26/2018 09:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.