Loading...

Simba SC yaisambaratisha Mbao FC


Klabu ya soka ya Simba leo imefanikiwa kuendelea kutanua wigo wa alama kileleni baada ya kupata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbao FC kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Mabao ya SImba yalifungwa na Shiza Kichuya dakika ya 37 kabla ya Okwi kufunga bao la pili dakika ya 40 kupitia mkwaju wa penati kufuatia kuangusha kwenye eneo la 18 na mlinzi wa Mbao FC.

Kipindi cha pili Okwi aliongeza bao la tatu dakika 69 lakini baadae aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavugo. Bao la nne la Simba lilifungwa na Erasto Nyoni kabla ya Asamoah Gyan kufunga bao la tano.

Kwa upande wake mshambuliaji Emmanuel Okwi raia wa Uganda amefikisha mabao 16 akiongoza orodha ya wafungaji msimu huu mbele ya Obrey Chirwa mwenye mabao 11 na John Bocco mwenye mabao 10.

Kwa ushindi huo sasa Simba imefikisha alama 45 kileleni na mabao 46 katika michezo 19, juu ya Yanga yenye alama 37 katika michezo 18 ikiwa katika nafasi ya pili.
Simba SC yaisambaratisha Mbao FC Simba SC yaisambaratisha Mbao FC Reviewed by Zero Degree on 2/26/2018 08:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.