Loading...

Real Madrid wameamua kumuuza nyota huyu mwishoni mwa msimu


Kwa mujibu wa ripoti za nchini Uhispania, klabu ya Real Madrid imeamua kumuuza Isco mwisho wa msimu huu.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 alikubali kuongeza mkataba wa miaka mitano na Real Madrid mwezi Septemba, ambao utamfanya aitumikie klabu hiyo hadi mwaka 2022.

Hata hivyo, kiungo huyo amekuwa na wakati mgumu sana kupata nafasi katika kikosi cha Madrid msimu huu, ambapo klabu hiyo iko nyuma ya vinara wa La Liga, FC Barcelona kwa pointi 19 kwenye msimamo.

Kwa mujibu wa taalifa ya Televisheni ya Uhispania ‘El Chiringuito’, Real Madrid inatarajiwa kumuuza kiungo huyo kwenye majira ya joto. 

Isco akiwa na meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane
Taarifa hiyo inadai kwamba, kama Zinedine Zidane ataendelea kuinoa klabu hiyo hadi baada ya msimu huu kumalizika, Mfaransa huyo atamuuza Isco.

Taarifa hiyo pia imedai kuwa Zidane anahisi wachezaji wamemwangusha sana msimu huu na ameushauri uongozi wa Real Madrid usikilize ofa zitakazojitokeza kutaka wachezaji katika klabu hiyo.

Klabu ya Liverpool tayari imehusishwa na uhamisho wa Isco na inaweza kujaribu kumnasa raia huyo wa Uhispania arithi mikoba ya Philippe Coutinho.
Real Madrid wameamua kumuuza nyota huyu mwishoni mwa msimu Real Madrid wameamua kumuuza nyota huyu mwishoni mwa msimu Reviewed by Zero Degree on 2/08/2018 09:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.