RIPOTI: Rwanda, Tanzania vinara nchi zenye viwango vidogo vya rushwa Afrika Mashariki
Ripoti hiyo imeonesha kuwa kwa Afrika mashariki, Rwanda imeongoza kwa alama 55, Tanzania imekuwa nafasi ya pili na ya 103 duniani ambapo imepanda kutoka alama 32 mwaka 2016 hadi alama 36 mwaka 2017. Kenya imechukua nafasi ya tatu, Uganda nafasi ya nne na Burundi ikishika mkia.
Kwa bara la Afrika, nchi 10 zenye viwango vidogo vya vitendo vya rushwa ya kwanza ni Botswana, Rwanda, Namibia, Mauritius, Senegal, Afrika Kusini, Burkina Faso, Lesotho, Tunisia na ya kumi ni Ghana.
Kwa nchi kumi zilizoongoza duniani kwenye orodha hiyo nyingi ni kutoka barani Ulaya isipokuwa Canada ambayo inatoka Amerika ya Kaskazini.
Kwenye ripoti hiyo iliyohusisha nchi 180 imeonesha nchi za Afrika ndio zimeongoza kuwa na vitendo vya rushwa, ambapo kwenye nchi 10 zilizoshika mkia nchi 6 zinatoka Afrika.
Kwa taarifa zaidi juu ya ripoti iliyotolewa na shirika hilo la Transparency International BOFYA HAPA.
RIPOTI: Rwanda, Tanzania vinara nchi zenye viwango vidogo vya rushwa Afrika Mashariki
Reviewed by Zero Degree
on
2/22/2018 02:01:00 PM
Rating: