Loading...

Tanzia: Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ afiwa na mwanaye

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’
Wakati akiwa anaitumikia timu yake huko Shelisheli, nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amepatwa na msiba baada ya kufiwa na mwanaye.

Mwanaye ambaye alikuwa bado mchanga amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Cannavaro anatarajia kuwasili nchini leo akitokea Shelisheli ambako amekwenda kuitumikia Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya St Louis.

Yanga ilipata sare ya mabao 1-1 na kusonga mbele huku Cannavaro akicheza kwa dakika 90.
Tanzia: Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ afiwa na mwanaye Tanzia: Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ afiwa na mwanaye Reviewed by Zero Degree on 2/22/2018 01:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.