Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 1 Februari, 2018

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte
Nigel Winterburn amesema kuwa Conte anaweza kufukuzwa kazi Chelsea kabla ya kumalizika kwa msimu huu kama ataendelea kulalamikia utaratibu wa usajili katika klabu hiyo.

Antonio Conte amesifia jitihada zake katika klabu ya Chelsea, licha ya kukiri kwamba klabu yake inaweza isifanikiwe kumaliza ligi katika nafasi nne bora.

Matej Kovar ajiunga na klabu ya Manchester United akitokea FC Slovacko.

Oliver Giroud amesema kuwa Chelsea ni chaguo sahihi kwake baada ya kusaini mkataba na klabu katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa mezi Januari. (Sky Sports)

Manchester United bado inafikiria kuhusu mpango wa kumfanya Mauricio Pochettino kuwa meneja wa kudumu wa klabu yao, licha ya kumpa Jose Mourinho mkataba mpya wiki iliyopita.

Manchester City inabaki na nia yake ya kumsajili kiungo wa klabu ya Shakhtar Donetsk raia wa Brazil, Fred.

Baada ya juhudi za kumnasa Riyad Mahrez kugonga mwamba, huku Gabriel Jesus na Leroy Sane wakiwa nje kwa sababu ya majeruhi, Pep Guardiola ameamua kumpandisha Lukas Nmecha kwenye kikosi hca kwanza cha timu kutoka timu B. (Manchester Eevening News)

Aubameyang akiwa mazoezini katika klabu yake mpya
Aubameyang amefanya mazoezi peke yake akiwa chini ya usimamizi wa mkufunzi wake mpya, Arsene Wenger. 

Klabu ya Dortmund imehasika kwa ujio wa Michy Batshuayi, mabaye amejiunga na klabu hiyo kwa kutafuta nafasi kwenye kikosi cha timu yake ya taifa kwenye kombe la duni. 

Klabu ya Arsenal ijilaumu yenyewe kwa kushindwa kukamilisha uhamisho wa beki wa West Brom, John Evans. (Dail Mail)

Gerlad Pique anasema kuwa angestaafu kucheza soka kama klabu ya Barcelona isingempa ofa ya mkataba mpya.

Aubameyang anafurahia kuingia katika vitabu vya historia ya klabu ya Arsenal na kuungana na aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Borussia Dortmund, Henrikh Mkhitaryan.

Riyad Mahrez hakutokea kwenye mazoezini Leicester City, huku ripoti zikidai kuwa nyota huyo ameigomea klabu baada ya dili la uhamisho wake kwenda Manchester City kugonga mwamba. (ESPN)

Islam Slimani
Newcatle United imethibitisha kumdajili mshambuliaji wa klabu ya Leicester City, Islam Slimani kwa mkopo.

Klabu ya Everton imemsajili beki wa Manchester City, Eliaquim Mangala kwa mkopo.

Gus Poyet amesema kuwa klabu ya Chelsea haiwezi kumufukuza kazi meneja wake, Antonio Conte kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya klabu ya Barcelona ya Uhispania. (talkSport)

Gonçalo Guedes
Sergio Ramos amesema kuwa rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez ameandaa ofa kubwa sana kwa ajili uhamisho wa winga PSG, Gonçalo Guedes anayeichezea klabu ya Valencia kwa mkopo. (Don Balon)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 1 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 1 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/01/2018 01:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.