NECTA watangaza matokeo ya kidato cha nne, kuyaona bofya hapa
Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Charles Msonde ameeleza kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 7.22 huku watahiniwa 265 wakifutiwa matokeo kwa udanganyifu wakiwemo wanafunzi 136 waliofanya mtihani wa kujitegemea (Private Candidate) na 129 waliofanya mtihani wa shule (School Candidate).
“Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09% kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa 277,283 ambao ni asilimia 70.09% hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7.22,” alisema Msonde.
Amemtaja mwanafunzi aliyeongoza kitaifa kuwa ni Ferson Mdee kutoka Shule ya Sekondari Marian Boys.
KUANGALIA MATOKEO YOTE BOFYA KATIKA VIUNGANISHI HIVYO HAPO CHINI:
KUANGALIA MATOKEO YOTE BOFYA KATIKA VIUNGANISHI HIVYO HAPO CHINI:
NECTA watangaza matokeo ya kidato cha nne, kuyaona bofya hapa
Reviewed by Zero Degree
on
2/01/2018 08:25:00 AM
Rating: