Loading...

Wachezaji 10 waliosajiliwa kwa gharama ya juu zaidi Januari 2018


Wakati kukiwa na mazungumzo mengi juu ya uhamisho ulioambatana na kubadilishana wachezaji wawili, Alexis Sanchez na Henrikh Mkhitaryan, pia kulikuwa na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumiwa na - na kupokea na vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza.
Hapa chini ni wachezaji 10 waliosajiliwa kwa gharama ya juu zaidi:

1: Philippe Coutinho, kutoka Liverpool kwenda Barcelona - kwa pauni milioni 146




Baada ya jitihada za klabu ya Barcelona kugonga mwamba kwenye majira ya joto, hatimaye vigogo hao wa La Liga walifanikiwa kumpata mtu wao mwezi Januari. Kwa kulipia kiasi cha pauni milioni 146 walifanikiwa kumnasa Philippe Coutinho kutoka Liverpool. Ada hiyo ya uhamishi ilimfanya raia huyo wa Brazil kuwa mchezaji wa pili aliyeshajiliwa kwa gharama kubwa duniani, wa kwanza akiwa ni Neymar.

2: Virgil van Dijk, kutoka Southampton kwenda Liverpool - kwa pauni milioni 75



Liverpool walimsajili Virgil van Dijk kuongeza nguvu katika safu yao ya ulinzi. Klabu hiyo imekuwa na tabia ya kuwasajili wachezaji wa Southampton katika miaka ya hivi karibuni - lakini ada waliyolipa kwa ajili ya kumpata Van Dijk imemfanya raia huyo wa Uholanzi kuwa beki ghali zaidi duniani.

3: Pierre-Emerick Aubameyang, kutoka Borussia Dortmund kwenda Arsenal - kwa pauni milioni 60


Mshambuliaji huyo wa Gabon amefanikiwa kutua Emirates baada ya mvutano mkubwa uliowahusisha Olivier Giroud na Michy Batshuayi, ambapo klabu ya Arsenal ililazimika kulipia pauni milioni 60 kukamilisha dili la uhamisho wa straika huyo kutoka Borussia Dortmund.

4: Aymeric Laporte, kutoka Athletic Bilbao kwenda Manchester City - kwa pauni milioni 57



Baada ya kukataa kujiunga na Manchester City kwenye majira ya joto mwaka 2016, hatimaye Pep Guardiola alifanikiwa kumsajili Aymeric Laporte kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi katika klabu hiyo.

5: Cenk Tosun, kutoka Besiktas kwenda Everton - kwa pauni milioni 27



Klabu ya Everton imekuwa bize katika madirisha mawili ya usajili yaliyopita kutafuta nguvu mpya kwenye safu yao ya mbele na mwisho wa siku ikafanikiwa kumnasa nyota wa timu ya taifa ya Uturuki, Cenk Tosun kwa pauni milioni 27.

6: Lucas Moura, kutoka PSG kwenda Tottenham - kwa pauni milioni 25



Klabu ya Tottenham inaonekana kuwa imefanikisha dili zuri kwa kumnasa nyota wa timu ya taifa ya Brazil na Paris Saint-Germain, Lucas Moura.

7: Adrien Silva, kutoka Sporting kwenda Leicester City - kwa pauni milioni 22


Hatimaye Adrien Silva amejiunga na klabu ya Leicester mwezi Januari, baada ya kushindwa kufanya hivyo katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili mwezi Agosti mwaka 2017 kwa kuchelewa sekunde 14.

8: Theo Walcott, kutoka Arsenal kwenda Everton - kwa pauni milioni 20



Baada ya kuitumikia Arsenal kwa miaka 12, Theo Walcott ameanza ukurasa mpya mwezi Januari kwa kujiunga na klabu ya Everton kwa pauni milioni 20. Straika huyo aliifungia Arsenal magoli 108 lakini aliondoka kwa lengo la kupata kupata nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza.

9: Guido Carrillo, kutoka Monaco kwenda Southampton - kwa pauni milioni 19


Southampton imekuwa na wakati mgumu sana kufunga magoli msimu huu hivyo, halikuwa jambo la kushangaza sana kuona klabu hiyo inavunja rekodi yake kwa kusajili mshambuliaji mpya. Guido Carrillo amekuwa akihangaikia kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Monaco lakini atakuwa na matumaini ya kupata nafasi ya kutosha katika dimba la St Mary.

10: Emerson Palmieri, kutoka Roma kwenda Chelsea - kwa pauni milioni 17.6


Chelsea imekuwa katika msako wa beki wa kushoto kwa muda mrefu na hatimaye msako wao umeishia kwa Emerson Palmieri kutoka Roma.
Wachezaji 10 waliosajiliwa kwa gharama ya juu zaidi Januari 2018 Wachezaji 10 waliosajiliwa kwa gharama ya juu zaidi Januari 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/01/2018 07:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.