Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 9 Februari, 2018
Thomas Lemar |
Mbio za klabu ya Arsenal kuwania saini ya winga wa Monaco, Thomas Lemar kimeichochewa na kitendo cha klabu ya Liverpool kujitoa katika kinyang'anyiro hicho. (Star)
Real Madrid italazimika kulipia kiasi cha pauni milioni 115 ili kumnasa golikipa wa klabu ya Manchester United David de Gea.
Klabu ya Liverpool imeachana na mpango wake wa kutaka kumsajili winga wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milionu 90. (talkSport)
Sol Campbell amefanya mazungumzo ya awali na klabu ya Oxford United juu ya kibarua cha kukinoa kikosi chao.
Aliyekuwa mshambuliaji wa Leicester City, Hull City, na Nottingham Forest, Matt Fraytt ametangaza kustaafu soka akiwa na miaka 31.
Sulley Muntari amejiunga na klabu ya Deportivo La Coruna na kupewa muda wa majiribio katika klabu hiyo kabla ya kusaini mkataba wa kudumu.
Klabu ya Arsenal inatakiwa imnase Conte mara tu atakapoondoka Chelsea ili achukue nafasi ya Arsene Wenger, kwa mujibu wa Paul Merson.
Winga wa Leicester City, Riyad Mahrez atarejea mazoezini leo, huku klabu yake ikijiandaa kucheza dhidi ya Manchester City kesho Jumamosi. (Sky Sports)
Jack Wilsher |
Riyad Mahrez amepigwa faini ya pauni 240,000 na klabu ya Leicester City kwa kukosa mazoezini kwa muda wa wiki mbili, wakati meneja wa klabu hiyo, Claude Puel akithibitisha kuwa winga huyo ataikosa mechi ya Jumamosi dhidi ya Manchester City. (Telegraph)
Real Madrid wanakaribia kumnasa nyota wa Inter Milan na Timu ya Taifa ya Argentina, Mauro Icardi lakini ripoti zinadai kuwa kuna wachezaji watatu wenye majina makubwa katika klabu hiyo hawajafurahia mpango huo. (Don Balon)
West Ham, Leicester zitashindania saini ya winga wa klabu ya Manchester City, Patrick Roberts.
Katika hali ya utani, wakala wa Jorginho amesema kuwa mshambuliaji huyo wa Napoli anaweza kuitosa Ligi Kuu ya Uingereza - kwa sababu ya hali ya hewa.
Barnsley inafanya mpango wa kumsajili Darren Moore achukue nafasi ya Paul Heckingbottom. (Sun)
Meneja wa Timu ya Taifa ya Ujerumani, Joachim Low ndio chaguo la kwanza kwa Real Madrid katika orodha ya wanaowaniwa na klabu hiyo kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane.
Christian Pulisic |
Mbio za klabu ya Manchester United kuwania saini ya kiungo wa Borussia Dortmund, Christian Pulisic zimechochewa na kauli ya nyota huyo, aliyesema kuwa ni mhsabiki mkubwa wa klabu hiyo ya Uingereza.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ana uhakika kwamba, Jack Wilshere atakubali kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo.
Di Maria amekiri kuwa alikaribia kujiunga na klabu ya Barcelona akitokea PSG kwenye majira ya joto mwaka 2017 kabla ya dili la uhamisho wake kukwama.
Van Persie ameifungia Feyernoor goli la kwanza tangu arejee katika klabu hiyo mpema mwaka huu.
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza cha Kombe la Dunia kinatarajiwa kwenda mapumzikoni mwisho wa msimu huu kabala ya kuingia kambini kuelekea kwa michuano hiyo nchini Urusi mwaka 2018. (Daily Mail)
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza cha Kombe la Dunia kinatarajiwa kwenda mapumzikoni mwisho wa msimu huu kabala ya kuingia kambini kuelekea kwa michuano hiyo nchini Urusi mwaka 2018. (Daily Mail)
Liverpool, Manchester United na Chelsea zinashindania saini ya beki wa klabu ya Lazio na Timu ya Taifa ya Uholanzi, Stefan De Vrij.
Oguzhan Ozyakup |
Arsenal inasubiria uamuzi wa Oguzhan Ozyakup baada ya kutoa ofa ya mkataba kwa nahodha huyo wa Besiktas.
Manchester United inakaribia kuipata saini ya Fabinho baada ya Mbrazil huyo kudai kuwa muda wake katika klabu ya Monaco unaelekea ukingoni. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 9 Februari, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
2/09/2018 11:28:00 AM
Rating: