Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 12 Februari, 2018
Marcelo na Neymar wakiwa katika mazoezi ya timu ya taifa ya Brazil |
Kuondoka kwa Diego Costa ni pigo kubwa kwa klabu ya Chelsea, kwa mujibu wa meneja wa West Brom, Alan Pardew.
MKurugenzi mkuu wa klabu ya Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke amesema kuwa klabu hiyo inaweza kubakisha meneja wao wa sasa, Peter Stoger hadi msimu ujao. (ESPN)
Mshambuliaji wa klabu ya Wolves, Joe Mason anaweza kumfuata mchezaji mwenzake, Jack Price katika Ligi ya MLS.
Stefano Okaka hana muda mrefu katika kikosi cha Watford na klabu hiyo itatazamia kumuuza mshambuliaji huyo kwenye majira ya joto.
Kuna ishara ndani na nje ya uwanja zinazoonyesha kuwa David Moyes ataendelea kuinoa West Ham kwa muda mrefu. (Mirror)
Antonio Conte amekiri kuwa na wakati mgumu kuishawishi timu yake kila mara, muda wa usajili wa wachezaji unapofika.
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amekanusha taarifa zinazodai kuwa David de Gea ataondoka kwenda Real Madrid kwenye majira ya joto.
Pep Guardiola ana amini Kevi De Bruyne anaweza kuwa changamoto kubwa kwenye tuzo za Ballon d'Or mwaka huu endapo ataisaidia Manchester City kutwaa mataji makubwa.
Golikipa wa Bayern Munich, Sven Ulreich amesaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Ujerumani.
Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte anasema kuwa uvumi unaoenea kuhusiana na hatma yake Stamford Bridge hauwezi kuwaathiri wachezaji wake namna yoyote ile. (Sky Sports)
Alvaro Morata amesema kuwa atakuwa tayari kuondoka Chelsea, lakini akilini mwake imo klabu ya Real Madrid pekee.
Jose Mourinho anasema kuwa Newcastle walicheza kama wanyama katika mechi baina ya timu hizo mbili jana Jumapili, iliyoisha kwa Manchester United kupigwa goli 1-0.
Thibaut Courtois |
Real Madird itaelekeza nguvu kwenye uhamisho wa golikipa wa Chelsea, Thibaut Courtois baada ya kugundua kuwa itakuwa rahisi zaidi kumilisha uhamisho wake kuliko wa David de Gea kutoka Manchester United. (Talksport)
Meneja wa klabu ya West Brom, Alan Pardew atapeleka kikosi chake nchini Uhispani kwenye joto kwa ajili ya mazoezi, ikiwa ni harakati za kujaribu kuinusuru timu yake isishuke daraja.
Mustakabali wa maisha yajayo ya Toby Alderweireld katika klabu ya Tottenham uko shakani baada ya kuachwa nje ya kikosi cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kitakachocheza dhidi ya Juventus. (Telegraph)
Luis Enrique ameamua kufanya kazi ya umeneja katika Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao na anazisubiria Chelsea na Arsenal.
Luis Enrique ameamua kufanya kazi ya umeneja katika Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao na anazisubiria Chelsea na Arsenal.
Liverpool ina nafasi kubwa ya kuzipiku Manchester United na Tottenham kwenye mbio za kuwania saini ya Pinchi.
Mchezaji wa Livingston, Shaun Byrne alikimbizwa hosipitalini baada kuumia katika mechi yao dhidi ya Dunfermline. (Sun)
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho atahakikisha inaipiku Manchester City katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa Real Madrid, Isco.
Max Meyer |
Arsene Wenger amemtaja kiungo wa Schalke 04, Max Meyer kuwa ndiye chaguo lake la kwanza kwenye usajili wa majira ya joto. (Star)
Mwenyekiti mwenza wa klabu ya West Ham, David Sullivan atakuwa na maamuzi madogo wakati wa usajili, kwa mujibu wa meneja wa klabu hiyo, David Moyes. (Guardian)
Meneja wa Brighton, Chris Hughton hakuwahi kumuona Mathew Ryan akiwa anacheza kablya ya kumsajili. (Daily Mail)
Mshambuliaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Uhispania, Fernando Llorente anahofia hatma yake katika klabu hiyo baada ya kukiri kuikosa Juventus.
Aliyekuwa nyota wa Tottenham na Newcastle, David Ginola anatarajia kupata mtoto katika umri wa miaka 51.
Rafael Benitez alishindwa kumnasa golikipa namba moja wa Uingereza, Joe Hart kuongeza nguvu katika orodha ya magolikipa na badala yake akamsajili Martin Dubravka.
Meneja wa Brighton, Chris Hughton hakuwahi kumuona Mathew Ryan akiwa anacheza kablya ya kumsajili. (Daily Mail)
Klabu ya Chelsea inaangalia uwezekano wa kumfukuza kazi Antonio Conte na kumpa aliyekuwa meneja wa Watford, Marco Silva mkataba wa muda Stamford Bridge.
Manchester City inakaribia kuwasajili wachezaji wawili wanaotarajiwa kung'ara kwa baadae - mmoja ni beki wa timu ya taifa ya Uholanzi chini ya miaka 20, Philippe Sandler anayeichezea PEC Zwolle na mwingine ni kiungo wa Paris Saint-Germain, Claudio Gomes.
Cenk Tosun |
Meneja wa Everton, Sam Allardyce anasema kuwa Cenk Tosun, aliyesajiliwa na klabu yake atachukuwa muda mrefu kuizoea Ligi Kuu ya Uingereza kutokana na hali ya hewa ya ubaridi. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 12 Februari, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
2/12/2018 12:22:00 PM
Rating: