Loading...

26 wafariki dunia na wengine 9 kujeruhiwa katika ajali ya Lori na Hiace Mkuranga

Twasira iliyokuwepo eneo la ajali mara baada ya ajali hiyo usiku
WATU 26 wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa baada ya gari dogo (Hiace) lililokuwa likitoka Mkuranga kuelekea Kimanzichana mkoani Pwani, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba chumvi likitokea Mtwara kuelekea Dar es Salaam.

Tela la lori lililokuwa limebeba chumvi likiwa limanguka na kupinduka kando ya barabara baada ya ajali hiyo
Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 25, 2018 kijiji cha Mparange Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani

Kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Kibiti, Mohamed Likwata, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba majeruhi wote wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Wakati huohuo, Rais John Magufuli amemtumia Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, rambirambi kutokana na vifo vya watu 26 vilivyotokea wilayani Mkuruganga.
26 wafariki dunia na wengine 9 kujeruhiwa katika ajali ya Lori na Hiace Mkuranga 26 wafariki dunia na wengine 9 kujeruhiwa katika ajali ya Lori na Hiace Mkuranga Reviewed by Zero Degree on 3/25/2018 11:54:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.