Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 25 Machi, 2018

Messi na Iniesta
Kama Andres Iniesta ataondoka Barcelona kwenye majira ya joto, Lionel Messi atakuwa nahodha Nou Camp. (Marca)
 
Ugomvi wa Paul Pogba na Jose Mourinho umefikia hatua mbaya kiasi kwamba mazungumzo yao yanapitia kwa meneja msaidizi, Rui Faria.

West Ham inapanga kumsajili nahodha wa klabu ya Newcastle, Jamaal Lascelles kwa pauni milioni 15 kwenye majira ya kiangazi.

Manuel Pellegrini ndio chaguo la kwanza kwa klabu ya West Ham kuchukua nafasi ya David Moyes kwenye majira ya kiangazi.

Aliyekuwa kocha wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel yuko kwenye mazungumzo na klabu ya Arsenal kuhusiana na kuchukuwa nafasi ya Arsene Wenger kwenye majira ya joto baada ya kukataa dili la kuinoa Bayern Munich.

Klabu ya Southampton bado inamhitaji David Wagner mwishoni mwa msimu licha ya kumwajiri Mark Hughes mwezi huu. (Sun)

Marcos Llorente
Marcos Llorente ataondoka Real Madrid kwenye majira ya joto baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo. (AS)

Jose Mourinho anacheza na hisia za mashabiki kwa Paul Pogba na Luke Shaw kwa sababu haamini kama mchezaji anaweza kumsababishia afukuzwe katika klabu ya Manchester United.

Brendan Rodgers amekiri kushawishika na kurejea ligi kuu ya Uingereza, huku kukiwa na klabu kama Arsenal ambayo imeonyesha nia ya kutaka huduma ya kocha huyo. (Daily Mail)

Chelsea na Arsenal zinatarajiwa kuingia kwenye ushindani mkubwa kuwania saini ya golikipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak kwenye majira ya joto.

Wakala mwenye jina kubwa, Mino Raiola amesema meneja wa Manchester City, Pep Guardiola ni mwoga na kudai kwamba hatapeleka mteja wake yeyote katika klabu hiyo. (Express)

Manchester United inapanga kuwasajili Raphael Varane, Toni Kroos, Marquinhos, Marco Verratti na Alex Sandro - na wako tayari kumuuza Paul Pogba kwa lengo la kuingiza fedha za kufanikishia mchakato huo.

Mohamed Salah
Mohamed Salah atakataa ofa yoyote kutoka Real Madrid na yuko tayari kusaini mkataba mpya wa pauni 200,000 kwa wiki na klabu ya Liverpool.

David Moyes atabakia kuwa meneja wa West Ham msimu ujao - lakini kama tu ataisaidia klabu hiyo kuepuka kushuka daraja Ligi Kuu ya Uingereza.

Liverpool italazimika kumlia Emre Can pauni 200,000 kwa wiki kama watahitaji kumshawishi abaki Anfield, huku Manchester City na Juventus zikiwa na hamu ya kumsajili kungo huyo wa Ujerumani.

Klabu ya Everton ina mpango wa kumsajili Chris Smalling kwenye majira ya joto, ambaye siku zake za kuendelea kuitumikia Manchester United zinaelekea mwisho. (Mirror)

Jamie Vardy anatarajiwa kuanza kama mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza wakati timu hiyo itakapocheza dhidi ya Italia siku ya Jumanne.

Angalau mchezaji mmoja wa Uingereza anafikiria kuajiri kampuni ya ulinzi kwa ajili ya kuilinda familia yake kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi kwenye majira ya kiangazi. (Telegraph)

Antonio Conte
Antonio Conte amefanya mazungumzo na klabu ya PSG juu ya kwenda kukinoa kikosi cha klabu hiyo akitokea Chelsea kwenye majira ya joto, kuku Unai Emery akiwa njiani kuondoka katika klabu hiyo ya Ufaransa mwishoni mwa msimu huu.

Gareth Southgate anatarajiwa kufanya mabadiliko kwenye kikosi cha timu ya taifa ya uingereza katika mechi yao ya kirafiki dhidi ya Italy, Jack Butland, Dele Alli na Eric Dier wakitegemewa kuanza na kikosi cha kwanza. (Observer)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 25 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 25 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/25/2018 11:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.