Loading...

Aliyepasuliwa ubongo kimakosa nchini Kenya azungumza


Mwanamume ambaye alifanyiwa upasuaji wa ubongo kimakosa nchini Kenya ameruhusiwa kuondoka hospitalini na kuzungumzia masaibu yaliyompata.

Akiwa na alama kubwa kichwani, Samwel Kimani aliiambia televisheni ya NTV kuwa, alikuwa amepoteza fahamu wakati alilazwa hospitalini na hakufahamua kilichosababisha madaktari kumfanyia upasuaji.
Hospitali ya Kenyatta iliomba msamaha baada ya kukiri kuwa vifaa vya kutambua wagonjwa hao wawili vilikuwa vimechanganyika.

Mwanamume ambaye alistahili kufanyiwa upasuaji wa ubongo kufuatia kuganda kwa damu naye aliruhusiwa kurudi nyumbani lakini bado haijulikani ikiwa anahitaji kufanyiwa upasuaji huo.

Kisa hicho kimewashangaza wakenya wengi tangu kiibuke na kilisababisha afisa Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta nchini Kenya kutumwa kwenye likizo ya lazima.
Hatua ya kumtuma Lilly Koros kwenye likizo ya lazima ilitangazwa na Waziri wa afya Sicily Kariuki ambaye alisema hatua hiyo ilikusudiwa "kupisha uchunguzi".

Mmoja kati yao wagonjwa hao ndiye alihitaji upasuaji wa kichwa ili kuondoa damu iliyokuwa imeganda kwenye ubongo wake.

Huyo mwingine alikuwa amefura kwenye kichwa lakini alihitaji matibabu ambayo hayakushirikisha upasuaji.

Lakini asiyehitaji upasuaji ndiye aliyeishia kufanyiwa upasuaji. Madaktari waligundua kosa hilo saa chache baada yao kuanza upasuaji walipogundua kwamba hawakuweza kuiona damu iliyoganda kwenye ubongo wa mgonjwa waliokuwa wanamfanyia upasuaji.
Aliyepasuliwa ubongo kimakosa nchini Kenya azungumza Aliyepasuliwa ubongo kimakosa nchini Kenya azungumza Reviewed by Zero Degree on 3/08/2018 05:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.