Loading...

Nani atatwaa taji la Ligi ya Mabingwa 2017/18? Ferdinand, Lampard na Gerrard watoa maoni yao


Rio Ferdinand, Frank Lampard na Steven Gerrard wamekubaliana juu ya nani atanyakua taji la Ligi ya Mabingwa.

Kwa upande wao. mashujaa hao wa zamani katika soka, Rio Ferdinand, Frank Lampard na Steven Gerrard wanaipa nafasi kubwa klabu ya Real Madrid kushinda taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Klabu hiyo ya Uhispania ilishinda taji hilo msimu uliopita kwa kuichapa Juventus goli 4-1 mjini Cardiff na kuendelea katika hatua ya robo fainali siku ya Jumanne baada ya kuitoa Paris Saint-Germain kwenye michuano hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya BT Spory, wakongwe hao wanadai Real Madrid iko nyuma ya vinara wa La Liga, Barcelona kwa pointi 15 kwenye msimamo. Lakini timu yao inaendelea kufanya mambo makubwa barani Ulaya na imejitoa kuhakikisha inatetea taji la Ligi ya Mabingwa.

Walipoulizwa ni nani atatwaa taji la Ligi ya Mabingwa, walisema:

Rio Ferdinand: “Real Madrid, kwa sababu ya uzoefu mkubwa na uwepo wa Ronaldo utachangia.”

Steven Gerrard: “Liverpool wana nafasi lakini Real Madrid ndio namba moja.”

Frank Lampard: “Inanilazimu kukubaliana na mawazo hayo lakini bado ni vigumu sana kuweza kutabiri mshindi.”
Nani atatwaa taji la Ligi ya Mabingwa 2017/18? Ferdinand, Lampard na Gerrard watoa maoni yao Nani atatwaa taji la Ligi ya Mabingwa 2017/18? Ferdinand, Lampard na Gerrard watoa maoni yao Reviewed by Zero Degree on 3/08/2018 06:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.