Loading...

EPL: Rekodi 6 za kifahari zitakazovunjwa na Manchester City 2017/18


Manchester City katika msimu wa 2017/18 inazungumzwa kama timu kubwa ambayo haijawahi kuonekana Uingereza.

Timu hiyo ambayo iko chini ya uongozi wa Pep Guardiola imejihakikishia nafasi ya kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza tangu ilipoanza kucheza bila kupoteza mchezo mwanzoni wa majira ya mvua ndogondogo (vuli). Hadi kufikia mwisho wa msimu, timu hii pia itakuwa imeandika jina lake katika kila kona ya vitabu vya rekodi.

Hapa chini tumekuweka rekodi sita za kifahari ambazo timu hiyo inatarajiwa kuzivunja kwenye Ligi Kuu ya Uingereza...

6. Kushinda Taji Mapema zaidi (Rekodi ya sasa: Mechi 5 zikiwa zimesalia, iliyowekwa na Manchester United msimu wa 1999/00)

Manchester United iliongoza msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kutwaa taji la ligi hiyo mwaka 1999 katika mechi yao ya 33, huku zikiwa zimesalia mechi tano kabla ligi haijafikia kikomo.

Man City wanaweza kufanya hivyo katika mechi yao ya 32 msimu wa 2017/18, ikiwa na maana watakuwa wamebakiza mechi sita. Kwa kushinda mechi mbili zaidi, kila kitu kitakuwa kimebadilika tayari.

Hiyo inaanzia kwa mchezo wao wa ugenini dhidi ya Everton mwezi huu baadaye, huku mechi ya 32 ikiwa ni ya mahasimu wao wa Manchester dhidi ya United katika dimba la Etihad tarehe 7 Aprili.

5. Tofauti kubwa ya pointi kwenye jedwali (Rekodi ya sasa: Pointi 18, iliyowekwa na Manchester United mmsimu wa 1999/00)

Kwa kuweka rekodi ya kushinda taji zikiwa zimesalia mechi tano, United pia ilimaliza ligi msimu wa 1999/00 kukiwa na tofauti ya pointi 18 mbele ya klabu ya Arsenal, ambayo ilishika nafasi ya pili.

Kwa sasa Manchester City inaongoza ligi kuu kwa tofauti ya pointi 16 zaida na bado ina nafasi ya kuongeza tofauti hiyo endapo Manchester United, Liverpool na Tottenham zitapoteza pointi katika michezo iliyosalia katika msimu huu wa 2017/18.

4. Magoli mengi (Rekodi ya sasa: Magoli 103, iliyoweka na Chelsea msimu wa 2009/10)

Manchester City ilikaribia kuvunja rekodi hii katika msimu wa 2013/14 wakati iliposhinda taji la Ligi Kuu kwa mara ya mwisho baada ya kumaliza wakiwa na idadi ya magoli 102 katika mechi 38 chini ya uongozi wa Manuel Pellegrini.

Liverpool, ambayo ilifunga magoli 101 katika msimu huo kwa msaada wa Luis Suarez na Daniel Sturridge, ni timu nyingine ambayo ilifanikiwa kumaliza ligi ikiwa na magoli zaidi ya 100 katika historia ya Ligi Kuu.

Manchester City lazima ifunge magoli 19 katika michezo yao nane iliyosalia ili kuvunja rekodi hiyo, ikihitaji wastani wa magoli 2.38 kwa kila mechi ambapo kwa sasa ina wastani wa magoli 2.83.

3. Tofauti nzuri ya magoli (Rekodi ya sasa: Magoli +71, iliyoweka na Chelsea msimu wa 2009/10)

Sio jambo la kushangaza kwa Chelsea kuweka rekodi ya kumaliza ligi ikiwa na magoli mengi zaidi sambamba na rekodi ya tofauti nzuri ya magoli katika msimu wa 2009/10.

Manchester City tayari iko kwenye nafasi nzuri kuweza kuvunja rekodi hiyo, kwa sasa inahitaji kuongeza magoli saba pekee kwenye hesabu yao ya sasa ya +65 kufikia tofauti ambayo haijawahi kufikiwa kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Tofauti ya magoli ya Manchester City katika ushindi wao wa Ligi Kuu msimu wa 2013/14 ilikuwa +65.

2. Kushinda mechi nyingi (Rekodi ya sasa: Mechi 30, iliyoweka na Chelsea msimu wa 2016/17)
Rekodi hii iliwekwa na Chelsea chini ya uongozi wa Antonio Conte msimu uliopita lakini inaelekea kuvunjwa msimu huu.

Manchester City imeshinda mechi 26 kati ya mechi zao 30 hadi hivi sasa katika msimu huu wa 2017/18 na hivyo inahitaji kushinda mechi nyingine tano katika mechi zao nane zilizobakia ili kuvunja rekodi hii.

1. Kumaliza na pointi nyingi (Rekodi ya sasa: Pointi 95, iliyoweka na Chelsea msimu wa 2004/05)

Wakati ambapo Manchester City inaweza isiwe na matumaini ya kuifikia rekodi ya magoli katika msimu mmoja wa Ligi Kuu ya Uingereza, iliyowekwa na klabu ya Chelsea katika msimu wa 2004/05, iko njiani kufikia rekodi ya pointi ambayo iliwekwa katika msimu huo.

Chelsea ilifanikiwa kumaliza na jumla ya pointi 95 katika msimu wa kwanza chini ya uongozi wa Jose Mourinho Stamford Bridge na kwa sasa Man City wamebakiza pointi 15 kuandika rekodi mpya, zikiwa zimesalia pointi 24 za michezo nane.

Kwa kutazama wastani wao wa pointi 2.7 kwa mechi hadi hivi sasa, Manchester City wako kwenye nafasi nzuri ya kuweza kuvunja rekodi hiyo na hata kuwa timu ya kwanza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kufikisha pointi 100 katika msimu mmoja. Kwa makadirio ya pointi kutoka katika michezo yao 30 ya awali msimu huu wa 2017/18, Man City wanakuwa kwenye nafasi ya kumaliza na pointi 102.
EPL: Rekodi 6 za kifahari zitakazovunjwa na Manchester City 2017/18 EPL: Rekodi 6 za kifahari zitakazovunjwa na Manchester City 2017/18 Reviewed by Zero Degree on 3/21/2018 08:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.