Loading...

Lori la mafuta lawaka moto na kusababisha vifo vya watu wawili mkoani Singida


Lori la mafuta limeanguka na kuwaka moto katika eneo la Mlima Sekenke, Misigiri, Wilaya ya Iramba Barabara ya Singida – Nzegana ambapo watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Deborah Magiligimba, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa nne na nusu asubuhi na kueleza kuwa watu wawili wamefariki, lakini bado hawajapata majina yao.

Gari iliyohusika kwenye ajali hiyo ni namba T167 DTC aina ya Flight Liner ambayo ilikuwa na Trailer namba T 960 ALS mali ya Petromac Africa Dar es Salaam ambalo liliacha njia na kupinduka hivyo kulipuka na kusababisha moto mkubwa uliopelekea vifo vya watu ho wawili ambao ni wanaume.

Uchunguzi wa jeshi la Polisi wa awali baada ya kufatilia kwenye mzani wa Singida, gari ilipimwa mzani wa Singida saa 1:27 asubuhi, dereva alikua anaitwa Erasto Abedi Rusazi na alikuwa na tingo msaidizi wake anayeitwa Ramadhani Hashim Ramadhini wote ni Wakazi wa Tabata Dar Es Salaam.

RPC Deborah Magiligimba, ametoa wito kwa madereva watii sharia za barabarani ili kuepusha ajali.






Lori la mafuta lawaka moto na kusababisha vifo vya watu wawili mkoani Singida Lori la mafuta lawaka moto na kusababisha vifo vya watu wawili mkoani Singida Reviewed by Zero Degree on 3/23/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.