Loading...

Goli la Kapombe, Algeria Vs Stars lazua gumzo


Kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, jana kimepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Algeria, mchezo ukipigwa Algiers nchini humo.

Mchezo huo ulimalizika kwa Taifa Stars kuendelea kuwa mteja dhidi ya Waarabu hao kwa kukubali kichapo cha mabao 4-1.

Kupoteza kwa mechi hiyo kumeleta gumzo kubwa hivi sasa juu ya bao ambalo mchezaji Shomari Kapombe alijifunga likiwa ni la pili kwa Algeria.

Kapombe alijifunga bao hilo kwa kichwa akiwa katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Mshambuiaji wa Algeria huku ikiwa imesalia dakika moja kuelekea mapumziko.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimuongelea Kapombe kwa kila namna wanavyofikiria kutokana na namna alivyojifunga bao hilo.

Wengi wameandika kwa namna wanavyojisikia juu ya Kapombe kwa kutupia vijembe vingi kuridhisha nafsi zao.

Wapo pia wanaochukulia kama kejeli na kusahau kama ni sehemu ya mchezo wakionesha utani.

Mabao ya Algeria katika mchezo huo ambao waliutawala kwa asilimia kubwa, yalifungwa na Baghdad Bounedjah kwenye dakika za 13 na 80, Shomari Kapombe akijifunga kwa kichwa dakika ya 43 na bao la mwisho likifungwa na Carl Medjan (52').

Bao pekee la Taifa Stars lilifungwa na Simon Msuva kufuatia kona safi ya Shiza Kichuya mnamo dakika ya 20.
Goli la Kapombe, Algeria Vs Stars lazua gumzo Goli la Kapombe, Algeria Vs Stars lazua gumzo Reviewed by Zero Degree on 3/23/2018 12:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.