Loading...

Mamlaka ya hali ya hewa [TMA] yatoa tahadhari


Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa hali mbaya ya hewa katika maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara ndani ya saa 24 kuanzia leo.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo na kudai kutakuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa ambazo zinatarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Singida, Dodoma, Morogoro, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe, Kilimanjaro, Manyara na Arusha


Mbali na hilo, TMA imesema kutakuwepo upepo mkali unaofikia kilomita 30 kwa saa kutoka Kaskazini- Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutokaa Kaskazini-Magharibi kwa Pwani ya Kusini huku hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi.

Taarifa kamili hapo chini:

Mamlaka ya hali ya hewa [TMA] yatoa tahadhari Mamlaka ya hali ya hewa [TMA] yatoa tahadhari Reviewed by Zero Degree on 3/11/2018 11:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.