Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 11 Machi, 2018

Rakitic na Neymar
Ivan Rakitic amesema kuwa yuko tayari kumpokea Neymar kwa mikono miwili kama nyota huyo wa PSG atahitaji kurejea Barcelona. (ESPN)

Mashabiki wa klabu ya Lille walivamia uwanjani na kuanza kuakimbiza wachezaji wa timu hiyo baada kutoka sare ya 1-1 na Montipellier.

Antonio Conte amesema kuwa Chelsea haiwezi kuvumilia kupoteza pointi nyingine kwenye mbio za kuwania taji la Ligi Kuu ya Uingereza.

Klabu ya Barcelona imekubali kumsajili Arthur Melo kutoka Gremio kwenye majira ya joto. (Sky Sports)

Manchester United iko tayari kumpa beki wa Juventus, Alex Sandro mara mbili ya mshahara wake wa sasa anaolipwa katika klabu hiyo ya Italia ili kumshawishi atue Old Traford.

Liverpool wanakaribia kukamilisha uhamisho wa golikipa wa klabu ya Stoke City na Uingereza, Jack Butland kwa pauni milioni 40..

Gareth Southgate anatarajia kuushangaza ulimwengu wa soka kwa kumuita golikipwa klabu ya Norwich, Angus Gunn kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.

Alex Iwobi ameanzisha mdaharo kwenye chumba cha kubadilishia nguo katika klabu ya Arsenal na anataka Arsene Wenger amrejeshe Thierry Henry.

Ruud Gullit amemwambia Antonio Conte kuwa anakabiliwa na kufukuzwa kazi katika klabu ya Chelsea kama hataifunga Barcelona wiki ijayo.

Borussia Dortmund wanata meneja wa Huddersfield na aliyekuwa meneja wao msaidizi, Wagner arejee kuinoa klabu yao.

Nyota wa Arsenal wanamtaka Arsene Wenger amlete hekaya wa klabu hiyo, Thierry Henry aongeze nguvu ya wachezaji kwenye mazoezi.

Andre Schurrle
Swansea na Crystal Palace zinawania kumrejesha Andre Schurrle katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Manchester United, Manchester City na Chelsea zinawania saini ya chupukizi wa klabu ya Heerenveen, Kik Pierie.

Klabu ya Brighton ina matamanio ya kumwajiri mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka Uingereza (FA), Dan Ashworth awe mkurugenzi wao wa kandanda. (Mirror)

Antoine Griezmann na mkewe walionekana pamoja wakikagua nyumba za kuishi Barcelona kuelekea uhamisho wake mkubwa kutoka Atletico Madrid kwenda kwa vigogo hao wa La Liga. (Marca)


Hatimaye Matej Delac anataka kuodnoka Chelsea kwenye majira ya joto baada ya kutumikia klabu hiyo kwa muda mrefu.

Manchester City iko hatarini kumpoteza mchezaji wao chipukizi, Dilrosun, ambaye anawaniwa na Newcastle na Swansea.

Crystal Palace wanafurahia kumruhusu Christian Benteke aende China kwa pauni milioni 20 kwenye majira ya joto.

Massimiliano Allegri
Meneja wa Juventus, Massimiliano Allegri yuko tayari kuinoa klabu ya Arsenal kama Arsene Wenger ataondoka kwenye majira ya joto.

Gareth Southgate anataka kuchagua magolikipa wanne wiki hii na ana mpango wa kumuita Nick Pope kikosini kwa mara ya kwanza. (Sun)

Meneja wa Watford, Javi Gracia hana uhakika kama Abdoulaye Doucoure atabakia katika klabu hiyo baada ya msimu huu. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 11 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 11 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/11/2018 12:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.