Loading...

N’Golo Kante aikana Paris Saint-Germain


N’Golo Kante anaonekana amechagua kusalia katika klabu ya Chelsea kwa kudai Stamford Bridge kwake yeye ni kama 'nyumbani', huku kukiwa na tetesi ambazo zinadai kuna vigogo wa barani Ulaya wanaitaka saini yake.

Kante alijiunga na Chelsea kwenye majira ya joto mwaka 2016 akitokea Leicester na amefanikiwa kuiteka safu ya kiungo, akiisaidia klabu yake kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza na kuonyesha uwezo mkubwa msimu huu wakati ambapo timu yake inapitia wakati mgumu.

Uwezo wake thabiti umepelekea ahusishwe na uhamisho kwenda PSG, lakini Kante kwa msistizo mkali amekanusha taarifa hizo.

Kwa mujibu wa taarifa ya The Evening Standard, Kante alisema: “Hapa niko nyumbani. Hii ndio klabu yangu hivyo, mimi bado ni mchezaji wa Chelsea na huu ni mwaka wangu wa pili nikiwa hapa.

“Baada ya kilichotokea msimu uliopita, ilikuwa ni jambo zuri kwetu sisi sote kwa sababu tulipata nafasi ya kusherehekea ubingwa. Kwenye msimu wa pili nilipata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa na tunaenda kumaliza ligi katika nafasi nne bora.”

Kwa sasa Chelsea iko nafasi ya tano kwenye jedwali la msima wa Ligi Kuu ya Uingereza.
N’Golo Kante aikana Paris Saint-Germain N’Golo Kante aikana Paris Saint-Germain Reviewed by Zero Degree on 3/20/2018 04:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.