Loading...

Nyamlani ateuliwa kukaimu nafasi ya Michael Wambura


Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokaa leo, imemteua Athumani Nyamlani kukaimu nafasi makamu wa rais wa shirikisho hilo.

Nyamlani ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, ameteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya Wambura kufungiwa maisha kujihusisha na soka.

Wambura amefungiwa na kamati ya maadili ambayo imeeleza kumkuta na hatia na makosa kadhaa yakiwemo ya kugushi nyaraka kwa ajili ya malipo ambayo yameelezwa hayakuwa sahihi.

Hata hivyo, tayari Wambura amekata rufaa kupinga hukumu hiyo akisisitiza, si sahihi hata kidogo.
Nyamlani ateuliwa kukaimu nafasi ya Michael Wambura Nyamlani ateuliwa kukaimu nafasi ya Michael Wambura Reviewed by Zero Degree on 3/25/2018 12:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.