Loading...

Neymar kuzigonganisha klabu hizi za EPL

Neymar Jr
Kwa mara nyingine tena Neymar anahusiswa na uhamisho mwingine baada ya miezi nane tangu ajiunge na Paris Saint-Germain. PSG walilipa pauni milioni 200 kumnasa nyota huyo, na kuufanya uhamisho huo kuwa wa gharama zaidi katika historia ya soka.

Lakini hivi karibuni Neymar amekuwa akihusishwa na kuondoka katika klabu hiyo ya Ufaransa. Wakati PSG ikiendelea kufanya vibaya Ulaya tena, baada ya kutolewa na Real Madrid katika hatua ya 16 bora, raia huyo wa Brazil anatazamia kujiunga na klabu kubwa kwa lengo la kujaribu uwezo wake.

Kwa mujibu wa taarifa ya 'Mundo Deportivo', Manchester City iko ayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha kumleta nyota huyo Uingereza. Inadaiwa kuwa Neymar anatamani kucheza chini ya Pep Guardiola. Mhispania huyo aliondoka Barcelona mwaka mmoja kabla Mbrazil huyo hajatua Camp Nou na wawili hao hawakufanikiwa kufanya kazi pamoja, lakini kwa heshima ya Guardiola, Neymar anatamani kufanya naye kazi.

Inaaminika kuwa Manchester United nao pia wako kwenye mbio za kuwania saini ya nyota huyo wa PSG. Kwa mujibu wa tovuti ya 'Diario Gol', Jose Mourinho anamtaka nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 na yuko tayari kumtoa Paul Pogba kwa vigogo hao wa Ufaransa ili ampate.

Hata hivyo, PSG wako tayari kufanya lolote kumbakisha Neymar nchini Ufaransa hata kama itakuwa ni kwa kubadilisha meneja.
Neymar kuzigonganisha klabu hizi za EPL Neymar kuzigonganisha klabu hizi za EPL Reviewed by Zero Degree on 3/25/2018 04:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.