Loading...

Nyota wa Barcelona atishia kuondoka Nou Camp


Kwa mujibu wa ripoti zilizotoka nchini Uhispania, Samuel Umtiti ametishia kuondoka Nou Camp.

Chanzo kikubwa kinaonekana kuwa ni mshahara, ambapo Barcelona inasita kukidhi mahitaji ya Mfaransa huyo wakati Manchester United wanaonekana kuwa na matamanio makubwa ya kumnasa beki huyo.

Jose Mourinho ameweka wazi tamaa yake ya kuimarisha safu yake ya ulinzi wakati dirisha la usajili kwenye majira ya joto litakapofunguliwa mwisho wa msimu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 53, na Mourinho nia ya kumshawishi beki huyo atue Old Trafford.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Umtiti alikataa kumjibu mwandishi wa habari wakati alipoulizwa ikiwa atasaini mkataba mpya Barcelona na kama atatimkia Manchester United.

Samuel Umtiti
Kuna shaka pia ya kwamba, inawezeka Umtiti anaitumia Manchester United kupata mkataba wenye maslahi mazuri Barcelona.

Imeripotiwa kwamba Umtiti anaingiza pauni milioni 3.5 kwa mwaka katika klabu ya Barcelona, lakini Manchester United wako tayari kumpa pauni milioni 8 kwa msimu.
Nyota wa Barcelona atishia kuondoka Nou Camp Nyota wa Barcelona atishia kuondoka Nou Camp Reviewed by Zero Degree on 3/27/2018 02:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.