Kauli ya Mwigulu Nchemba yapingwa
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo Bisimba |
Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Dk. Nchemba alisema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi, ili kutengeneza hatima ya nchi.
“Wakati walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi, wapo watu wengine huwalalamikia tu, na hawajui kwamba kinachofanyika ni kwa manufaa yetu. Niwaombe kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni hivyo, ili kutengeneza taswira ya nchi yetu,” alisema Dk. Mwigulu.
- Soma na hii - Mwigulu ataka viboko vitumike inapobidi
“Wakati walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi, wapo watu wengine huwalalamikia tu, na hawajui kwamba kinachofanyika ni kwa manufaa yetu. Niwaombe kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni hivyo, ili kutengeneza taswira ya nchi yetu,” alisema Dk. Mwigulu.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo Bisimba, alisema kutumia fimbo kwa mwanafunzi hakuwezi kusaidia kumjengea nidhamu.
Pia, alisema kutumia adhabu hiyo kunaweza kuwa chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo yao kielimu.
Pia, alisema kutumia adhabu hiyo kunaweza kuwa chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo yao kielimu.
“Ni kweli kwamba walimu wanapaswa kuachwa watekeleze majukumu yao bila kuingiliwa, lakini linapokuja jambo la adhabu au kujenga nidhamu kwa wanafunzi lazima uangaliwe mfumo unaotumika,” alisema Dk. Kijo Bisimba na kuongeza:
- Soma na hii - Wanafunzi wacharaza viboko walimu
“Zipo adhabu ambazo mwanafunzi anaweza kupewa akikosa, lakini si kwa kuchapwa fimbo. Unaweza ukafikiri ukimchapa ndio unamjenga, lakini kumbe ndio unambomoa zaidi. Nasema hivyo kwa sababu unapoanza kumchapa mwanafunzi hawezi kufanya vizuri tena darasani. Mimi namuomba waziri a-deal (ashughulike) na mambo ya wizara yake, ya elimu ayaache.”
Kauli ya Mwigulu Nchemba yapingwa
Reviewed by Zero Degree
on
3/27/2018 01:55:00 PM
Rating: