Loading...

Rais akubali kujiuzulu kwa tuhuma za ubadhilifu

Ameenah Gurib-Fakim
Rais wa Mauritius, Ameenah Gurib-Fakim amekubali kuachia madaraka baada ya kutuhumiwa kutumia kadi ya benki yenye thamani ya dola za kimarekani elfu kumi iliyotolewa na shirika la msaada katika matumizi yake binafsi.

Rais huyo ataachia madaraka yake baada ya madhimisho ya miaka hamsini wa uhuru wa taifa lake wiki ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Reuters, rais huyo amekana kosa hilo na kudai kuwa alirudisha fedha zote.

Rais huyo aliyeingia madarakani mwaka 2015 alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa nchini Mauritius na ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kwenye madhimisho ya Marais wa Mauritus.

Waziri mkuu wa nchi hiyo, Pravind Jugnauth amewaambia waandishi wa habari kuwa rais Ameenah ataachia wadhifa wake kama ilivyopangwa na kuongeza kwa kusema kuwa kipaumbele cha taifa ndicho kilichozingatiwa ili taifa hilo liendelee kuwa nchi ya mfano.

Hata hivyo gazeti moja nchini humo lilichapisha uthibitisho wa nakala ambazo rais huyo alifanyia manunuzi ya vitu vyake vya thamani nchini Uingereza.
Rais akubali kujiuzulu kwa tuhuma za ubadhilifu Rais akubali kujiuzulu kwa tuhuma za ubadhilifu Reviewed by Zero Degree on 3/10/2018 01:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.