Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 10 Machi, 2018

Kylian Mbappe
Kylian Mbappe anasema kuwa alifanya uamuzi sahihi kujiunga na klabu ya PSG akitokea Monaco mwaka jana.

Meneja wa Bayern Munich, Jupp Heynckes amekanusha taarifa zinazodai kuwa atastaafu kazi hiyo kwenye majira ya joto.

Arsene Wenger: Mshabiki wa Arsenal wanamchukia meneja wa timu yao bali sio mimi. (ESPN)

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp anasisitiza kuwa klabu yake imejiandaa kutumia kiasi kikubwa cha fedha kuhakikisha inaunda kikosi chenye nguvu ya kupambana bila kuteteleka.

Mshambuliaji wa Rangers, Alfredo Morelos amesaini mkataba mpya katika klabu hiyo.

Marco Reus amesaini mkataba mpya na Borussia Dortmund utakaomfanya aitumikie klabu hiyo hadi mwaka 2023.

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amethibitisha kupata mtoto wa tatu wa kiume. (Sky Sports)

Real Madrid inaweza kuachana na mpango wa kuwasajili Davi de Gea na Thibaut Courtois baada ya kuhamishia mapenzi yao kwa golikipa wa timu ya taifa ya Croatia U21, Karlo Letica. (Marca)

Thomas Lemar
Manchester City wanatarajiwa kushtukiza usajili wa nyota klabu ya Monaco, Thomas Lemar kwenye majira ya joto. (Telegraph)

Manchester United wana mpango wa kumsajili beki wa klabu ya Borussia Dortmund, Sokratis Papastathopoulos kama watashindwa kumnasa beki wa Tottenham, Toby Alderweireld kwenye majira ya joto.

Joe Hart atapewa nafasi ya kufufua ndoto zake za kushiriki Kombe la Dunia kwa mara nyingine tena katika mechi ya West ham dhidi ya Burnley. (Mirror)

Gianluigi Donnarumma
Golikipa wa AC Milan, Gianluigi Donnarumma anatarajiwa kuondoka kwenye majira ya joto baada ya klabu hiyo kuanza mkakati wa kumsajili golikipa namba moja wa klabu ya Napoli, Pepe Reina.

Uwanja wa soka mkubwa zaidi, wenye uwezo wa kubeba watazamaji 135,000 unatarajiwa kujengwa nchini Iraq, kama zawadi kutoka kwa mfalme wa Saudi Arabia, Salman. (Sun)

Klabu ya Manchester United inafanya mpango wa kumtoa Luke Shaw kama sehemu ya ofa kumnasa beki wa Tottenham, Danny Rose. (Daily Mail)

Chelsea wako tayari kufanya jambo lolote kuhakikisha wanamsajili beki wa klabu ya Barcelona, Samuel Umtiti kwenye majira ya joto.

David Moyes ameambia atapewa kiasi cha pauni milioni 60 kwa ajili ya usajili wa wachezaji wapya kama atafanikiwa kuibakisha klabu ya West Ham katika Ligi Kuu ya Uingereza. (Express)

Meneja wa klabu ya Swansea City, Carlos Carvalhal
Swansea inaaweza kukabiliana na ushindani mkubwa kumbakisha Carlos Carvalhal hadi msimu ujao. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 10 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 10 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/10/2018 11:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.