Loading...

Real Madrid kuitibulia Chelsea kwa nyota huyu wa Serie A


Real Madrid imegeukia kwa Edin Dzeko kwa lengo la kutibua mipango ya klabu ya  Chelsea.

Katika kutafuta mshambuliaji mzoefu, na hata wa ziada kulingana na jinisi soko litakavyokuwa, Real Madrid wanafanya mawasiliano na AS Roma wakitaka kujua kama raia huyo wa Bosnia bado yuko sokoni.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 aliyekaribia kutua Chelsea kwenye dirisha la usajili mwezi Januari, na ambaye pia aliwahi kuwa mshambuliaji wa Manchester City na Wolfsburg anaweza kuondoka Italia kwenye majira ya joto baada ya misimu mitatu.

Edin Dzeko
The Blues walishindwa katika jaribio lao la kumrejesha mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City kwenye Ligi Kuu ya Uingereza mwezi Januari baada ya raia huyo wa Bosinia kusita kutua Stamford Bridge na kuwa chaguo la pili la Antonio Conte katikati ya msimu.

Na sasa Real Madrid wanatamani kumnasa Dzeko, licha ya ripoti za magazeti Uhisapani kudai nyota huyo ameshakubali kutua Stamford Bridge kwenye majira ya joto.
Real Madrid kuitibulia Chelsea kwa nyota huyu wa Serie A Real Madrid kuitibulia Chelsea kwa nyota huyu wa Serie A Reviewed by Zero Degree on 3/26/2018 03:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.