Loading...

Romario kuwania ugavana Rio de Janeiro, Brazil

Romario de Souza
Seneta wa Brazil na mchezaji wa zamani Romario de Souza atawania wadhfa wa ugavana wa Rio de Janeiro mwezi Oktoba.

Jimbo hilo limekumbwa na ghasia na liko katika hatari ya kufilisika.

Mshindi huyo wa kombe la dunia la mwaka 1994 anayejulikana kama Romario anasema kuwa kampeni yake itaangazia kukabiliana na matatizo hayo.

Atakuwa mgombea wa chama cha mrengo wa kati cha Podemos. Amesifiwa kuwa seneta katika vita vyake dhidi ya ufisadi katika kandanda.

''Katika wakati huu wa ghasia, mabadiliko yanahitajika haraka. Rio ilikuwa na matatizo ya kiusalama, lakini sio kama sasa'' , mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 52 alisema siku ya Jumamosi akitangaza kuwania wadhfa huo.

''Sina uzoefu wa kusimamia. Itakuwa kutokana na majaliwa ya Mungu , kwa mara ya kwanza kuonyesha kwamba nimekuwa na fursa kuonyesha kile nilichojifunza katika maisha yangu''.


Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona kwa sasa anachunguzwa kwa madai ya kuficha mali yake kwa lengo la kukwepa kulipa deni, kulingana na vyombo vya habari vya Brazil.

Amekana madai hayo.
Romario kuwania ugavana Rio de Janeiro, Brazil Romario kuwania ugavana Rio de Janeiro, Brazil Reviewed by Zero Degree on 3/18/2018 04:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.