Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 2 Machi, 2018

James Rodriguez
Mkurugenzi wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha kwamba klabu hiyo itaangalia uwezekano wa kumsajili nyota wa Real Madrid, James Rodriguez moja kwa moja.

Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Barecelona hautawezekana kwa sababu "ndege haziruhusiwi kupaa juu ya nyumba ya Lionel Messii "kwa mujibu wa Rais wa kampuni ya ndege ya Vuielig, Javier Sanchez-Prieto. (Marca)

Jose Mourinho anategemea kumuona Zlatan Ibrahimovic akiondoka Manchester United mwishoni mwa msimu huu. 

Eliaquim Mangala anatarajiwa kuzikosa mechi zote za Everton zilizosalia msimu huu baada ya kufanyiwa uoasuaji wa goti, kwa mujibu wa Sam Allardyce.

Sol Campbell anasema kuwa anasubira uamuzi wa klabu ya Grimsby kuhusu nafasi ya umeneja katika klabu yao.

Sam Allardyce amekanusha tetesi zinazodai ataondoka katika klabu ya Everton mwishoni mwa msimu huu.

Arsene Wenger hatakuwa mkufunzi wa Arsenal msimu ujao, kwa ,ujibu wa Paul Merson. (Sky Sports)

Ivan Rackitic amieomba klabu ya Barcelona impe ufafanuzi juu ya nafasi yake kikosini msimu ujao, huku mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antonie Griezmann akitarajiwa kutua Nou Camp. (Dario Gol)
Marco Reus
Spurs iko tayari kujaribu kumsajili nyota wa Timu ya Taifa ya Ujerumani na klabu ya  Borussia Dortmund, Marco Reus.

Manchester United inatarajiwa kumsajili Willian kotoka Chelsea na Toni kross kutoka Real Madrid kwenye majira ya joto.

Rela Madrid ilikuwa na mpango wa kuwasajili Iniesta, Dani Alves na Cesc Fabregas mwaka 2008.

Golikipa wa klabu ya Chelsea, Thibaut Courtois anavutiwa na uhamisho kwenda PSG.

Manchester City inatarajiwa kumruhusu mshambuliaji wake, Olarenwaju Kayod ajiunge na Shakhtar Donetsk kwa mkopo, huku ikajairbu kukamilisha uhamisho wa kiungo wa klabu hiyo na Timu ya Taifa ya Brazil, Fred. (ESPN)

Mazungumzo juu ya mkataba mpya kati ya Courtois na klabu ya Chelsea yatafanyika kwenye majira ya joto (Sun)

Alan Pardew anakiri kuwa anaweza asipewe nafasi ya kupoteza mechi nyingine, huku ukiwa umebaki muda mchache kabla ya mchezo wao dhidi ya Watford.

Romain Saiss ana amini kuwa Wolves itarajea kwenye hali ya kawaida wikendi hii - baada ya kuwa na wiki ngumu ya mazoezi kwenye theluji.

Meneja wa klabu ya West Ham, David Moyes anaandaa pauni milioni 10 kwa ajili ya kumasa kiungo wa Bournemouth, Harry Arter baada kushindwa kumpata kiungo huyo kwa safari mbili kabla. (Express)

Manchester United imeungana na Liverpool kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Napoli, Jorginho, huku Jose Mourinho akiwa tayari kulipa paundi milioni 50 kwa ajili ya nyota huyo. (Star)

Wakala wa Mario Balotelli anasema kuwa mteja wake anaweza kurejea Ligi Kuu ya Uingereza kwenye majira ya joto. (Mirror)
Mario Lemina
Liverpool inatarajia kumnasa kiungo wa klabu ya Southampton na Timu ya Taifa ya Gabon, Mario Lemina. (L'Equipe)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 2 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 2 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/02/2018 01:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.