Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 28 Machi, 2018

Gabriel Jesus
Mshambuliaji wa Manchester City, Gabriel Jesus amekataa ofa ya mkataba mpya wenye thamani ya pauni 90,000 kwa wiki na kusitisha mazungumzo na klabu yake hadi kwenye Kombe la Dunia.

Mchezo wa kuvutia wa Bournemouth umeisaidia klabu hiyo kujipatia ongezeko la pauni milioni 7 kwenye ada ya maonyesho ya tetelevisheni. (Times)

Bodi ya klabu ya Barcelona inafikiria kuona kama kuna umuhimu wa kununua beki wa kati wa ziada kwenye majira ya joto, huku Matthijs de Ligt wa Ajax na Unai Nunez wa Athletic Bilbao wakiwa kwenye mipango yao.

Barcelona inataka kukamilisha uhamisho wa Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid mapema kwenye majira ya kiangazi.

Keylor Navas hataki kuondoka Real Madrid kwenye majira ya joto, hata kama klabu hiyo itasajili golikipa mwingine. (Mundo Derpotivo)

Manchester United watachunguza kilichotokea kati ya Jose Mourinho na nyota wawili wa zamani wa klabu ya Chelsea, Kevin De Bruyne na Mohamed Salah kabla ya kuamua hatima ya Luke Shaw.

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amefanya mazungumzo na wakala wa nyota  wa RB Leipzig, Timo Werner katika jaribio la kumshawishi mshambuliaji huyo atue Ligi Kuu ya Uingereza licha ya kuhusishwa na uhamisho kwenda klabu ya Real Madrid.

Beki wa Aston Villa, John Terry bado hajaamua kama ataichezea klabu hiyo msimu ujao kama itafanikiwa kupanda daraja. (Express)

Croatia haikumuita Luka Modric kwenye kikosi chao kilichoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mexico kwa sababu meneja wa timu ya taifa hilo, Zlatko Dalic na meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane walikubaliana kuwa kiungo huyo anahitaji mapumziko zaidi. (Marca)

Arsene Wenger amekiri kwamba anataka kuinoa timu nyingine kama ataondoka Arsenal kwenye majira ya kiangazi.

Fabio Capello 
Aliyekuwa meneja wa Uingereza, Fabio Capello ameibuka na kuwa kinara wa wagombea wa nafasi ya Arsene Wenger.

Gabriel Jesus yuko kwenye mgogoro na viongozi wa Manchester City baada ya kukataa ofa ya mkataba mpya aliyopewa hivi karibuni.

Liverpool wamejiandaa kuchomolea Bayern Munich kama itapeleka ofa yoyote kwa ajili ya Roberto Firmino, ambaye klabu hiyo inapanga kumwania kama Robert Lewandowski ataondoka kwenda Real Madrid.

Manchester United itazikabili Real Madrid na Paris Saint-Germain kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Lazio, Sergej Milinkovic-Savic.

Liverpool wamekaa mkao wa kula baada ya kiungo wa Watford, Abdoulaye Doucoure kukiri kwamba anatamani kuja kuichezea klabu hiyo. (Sun)

Hatima ya rais wa klabu ya Nice, Jean-Pierre Riviere na meneja mkuu, Julien Fournier iko shakani baada ya kutofautiana na wanahisa wa klabu. (L'Equipe)

Manchester United na Manchester City zitachuana vikali kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Nice na timu ya taifa ya Ivory Coast, Jean-Michael Seri.

Manchester City itaanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na Raheem Sterling baada ya msimu huu kumalizika. (ESPN)

Beki wa klabu ya Barcelona, Samuel Umtiti anatishia kuondoka kwenda Man United kwa dili la pauni milioni 53 isipokuwa kama vigogo hao wa La Liga watampa mkataba mpya wenye thamani ya pauni milioni 8 kwa msimu.

Golikipa wa klabu ya Manchester United, David De Gea anasema kuwa heshima anayopewa nchini Uingereza ni kubwa kuliko Uhispania.

Liverpool wamekubali kushindwa kwenye mbio za kuwania saini ya golikipa wa Roma, Alisson baada ya klabu ya Real Madrid kumwingiza Muitaliano huyo ndani ya mipango yao ya usajili kwenye majira ya joto.

Marcos Alonso
Beki wa klabu ya Chelsea, Marcos Alonso hana mpango wa kurejea Real Madrid mwishoni mwa msimu.

Meneja wa timu ya taifa ya Wales, Ryan Giggs amewazuia wachezaji wake kucheza gofu kwa kuhufia majeruhi. (Daily Mail)

Kiungo wa klabu ya Newcastle, Mikel Merino amekiri kuwa angependelea kurejea Uhispani siku zijazo, huku kukiwa na tetese zinazomhusisha na Athletic Bilbao.

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Uingereza (FA), Prince William, ataikosa fainali ya michuano ya FA kwa lengo la kuhudhuria kwenye harusi ya Prince Harry Mei 19. (Mirror)

Juventus itakabiliana na Manchester United kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya beki kutoka Valencia, Joao Cancelo baada ya nyota huyo kuonyeshwa uwezo mkubwa akiwa na Inter Milan kwa mkopo. (Star)

Timu zitakazoshiriki Ligi ya Mabingwa na Europa Ligi zitaruhusiwa kutumia wachezaji wapya waliosajiliwa, ambao wameshashiriki katika michuano hiyo wakiwa na timu zao za awali.

Arsenal ina matumaini kwamba Jack Wilshere, Alexandre Lacazette na Aaron Ramsey watakuwa fiti kuivaa Stoke City Jumapili.

Steve Cotterill ameikataa nafasi ya kuwa mkufunzi wa Scunthorpe. (Telegraph)

Thomas Lemar
Winga wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar anajaribu kuzirejesha Liverpool na Arsenal kwenye mbio za kuwania saini yake baada ya uhamisho wakek kwenda Ligi Kuu ya Uingereza kugonga mwamba mwanzoni mwa msimu. (Independent)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 28 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 28 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/28/2018 10:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.