Loading...

Wawili mbaroni kwa kuhamasisha maandamano


Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kupitia kwenye mitandao ya kijamii wakitumia simu zao za mikononi.

Kamanda wa polisi wa mkoa Dodoma Gilles Muroto amesema Watu hao wamekua wakisambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu kuandamana huku wakijua ni kosa kisheria.

Aidha Kamanda Mruto ametoa wito kwa watu kutofuata mkumbo kuhamasisha watu kufanya maandamano kwani ni kosa kisheria na kuwa yeyote ambaye atakamatwa atashughulikiwa kisheria

Mbali na hilo Kamanda Mruto amesema kuwa upelelezi ukikamilika watu hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao kuhusu kuhamasisha watu kufanya maandamano kupitia mitandao ya kijamii ambayo yamepangwa kufanyika April 26, 2018 nchi nzima na yakiratibiwa na mwanadada Mange Kimambi kupitia mitandao ya kijamii.
Wawili mbaroni kwa kuhamasisha maandamano Wawili mbaroni kwa kuhamasisha maandamano Reviewed by Zero Degree on 3/21/2018 01:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.