Loading...

AliKiba afunga ndoa na mpenzi wake mjini Mombasa


Nyota wa muziki wa Bongo nchini Tanzania Ali Saleh Kiba ameuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenziwe kutoka Kenya.

Harusi hiyo ya kukata na shoka iliofanyika katika msikiti wa Ummul Kulthum ilihudhuriwa na rafiki wa mwanamuziki huyo Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.



Mwanamuziki huyo wa wimbo wa Seduce me aliisafirisha familia yake mjini Mombasa siku moja kabla ya kumuoa mchumba wake.

Ni watu wachache pekee walioalikwa katika harusi hiyo iliodaiwa kufanyika kisiri.

Duru zimearifu kwamba sherehe nyengine ya kukata na shoka inatarajiwa kufanyika Aprili 26 mjini Dar es Salaam.
AliKiba afunga ndoa na mpenzi wake mjini Mombasa AliKiba afunga ndoa na mpenzi wake mjini Mombasa Reviewed by Zero Degree on 4/19/2018 01:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.