Loading...

Diamond, Nandy waomba radhi kwa yaliyotokea

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ (kulia) akiongea na wanahabari, pembeni ni msanii mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema kuwa kwa yale yote yaliomtokea ya kuachia video zilizokosa maadili kwenye mitandao ya kijamii amejifunza mengi na kwamba kilichotokea alikuwa hajui sheria za mitandao hivyo alikuwa akijipostia tu kumbe alichokuwa akiposti mashabiki walikuwa wakichukua na kuweka kwao kwa hiyo yaliyotokea avumiliwe.

Diamond aliyazungumza hayo leo Alhamisi alipoitwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) pamoja na msanii mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’ ambao wiki iliyopita video zao zilizokosa maadili zilisambaa mitandaoni.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa TCRA, Diamond alisema anajuta kitendo cha kuachia video hizo.

“Nimejifunza mengi, mimi siyo mtu wa kutafuta kiki, nimegundua mimi ni kijana mwenye mashabiki wengi mitandaoni nadhani kuliko kijana yeyote nchini, sasa wapo ambao wanajifunza kupitia mimi kwa hiyo niombe radhi kwa yote, ujana ni maji ya moto tumeelimishwa, hayatajirudia tena na naahidi nitakuwa balozi kwa vijana wenzangu kuhusu masuala ya mtandao,” alisema Diamond.

Naye, Nandy aliwaomba radhi watu wote juu ya matumizi mabaya ya mtandao.

Msanii, Faustina Charles ‘Nandy’ akiongea na wanahabari

“Naomba radhi kwa yote yaliotokea, nimejifunza mengi TCRA na tukio kama hilo halitakuja kutokea tena.”
Diamond, Nandy waomba radhi kwa yaliyotokea Diamond, Nandy waomba radhi kwa yaliyotokea Reviewed by Zero Degree on 4/19/2018 03:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.