Loading...

Diamond atiwa mbaroni kwa kusambaza video chafu, Nandy asakwa

Waziri Mwakyembe
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema kuna baadhi ya wasanii ambao walianza kufanya uhuni ndani ya mitandao akiwemo mwanamuziki nyota, Diamond Platinumz, ambaye tayari amekamatwa na polisi na anahojiwa kutokana na picha alizorusha mtandaoni.

Mwakyembe ameliagiza Jeshi la Polisi kumsaka msanii, Nandy ili naye ahojiwe kutokana na tuhuma kama hizo ambapo yeye video yake na Bil Nas ilisambaa mitandaoni wakijiachia kimahaba.

Mwakyembe amesema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyehoji akitaka kujua serikali ina mkakati gani kutokana na wimbi la wasanii kuachia video na picha zao utupu mitandaoni.

Akijibu swali la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga alilotaka ufafanuzi kuhusu watu maarufu wanaovunja maadili kwenye mitandao ya kijamii na kutoa lugha za matusi, Waziri Mwakyembe amesema wizara imeweka kanuni rasmi za kuweza kukabiliana na watu wanaovunja maadili hususan kwenye mitandao, ambapo tayari imempeleka mahakamani msanii mkubwa ambaye video zake za faragha zimevuja, na pia inakusudia kumpeleka polisi msanii wa kike Nandy.

“Tulitunga sheria toka mwaka 2010 lakini tulikosa kanuni, na sasa hivi tumeshaweka, na zimeshaanza kufanya kazi, jana tumempeleka mahakamani msaniii Diamond kwa video alizorusha, na pia Nandy itabidi apelekwe polisi kuhojiwa”, amesema Waziri Mwakyembe.

Aidha, Mwakyembe alisema Tanzania siyo kokoro la uchafu na kueleza kwamba wanaangalia taratibu za kuwafikisha Diamond na Nandy mahakamani kutokana na tuhuma hizo.

Waziri Mwakyembe ameendelea kwa kuwataka vijana kutotumia mitandao ya kijamii vibaya kwani mitandao sio kokoro ya kupeleka uchafu wowote, kwa kuwa nchi ina maadili na utamaduni wake na inapaswa kuulinda.
Diamond atiwa mbaroni kwa kusambaza video chafu, Nandy asakwa Diamond atiwa mbaroni kwa kusambaza video chafu, Nandy asakwa Reviewed by Zero Degree on 4/17/2018 11:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.