Loading...

Everton itazikabili Manchester United na Chelsea kumsajili straika huyu


Mshambuliaji wa Watford, Richarlison anawindwa na Manchester United, Chelsea pamoja na Everton.

Mbrazil huyo alikuwa na mwanzo mzuri katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, akifanikiwa kufunga magoli matano katika mechi 12 za mwanzo.

Hata hivyo, hajafanikiwa kufunga tangu mwezi Novemba na kwa mujibu wa Sky Sports, straika huyo wa Watford mwenye umri wa miaka 20 anajitahidi sana, kwa kucheza miezi 12 months bila mapumziko, mwanzo akiwa na Fluminense nchini Brazil, na sasa katika Ligi Kuu ya Uingereza tangu mwezi Agosti.

Richarlison ameichezea Watford michezo 36 msimu huu, mchezo wa hivi karibuni ulikuwa ni dhidi ya Burnley Jumamosi iliyopita.

Chelsea walijaribu kumsajili Mbrazil huyo kwenye majira ya joto mwaka jana, lakini nafasi ambayo alikuanayo kwenye kikosi cha kwanza chini ya aliyekuwa meneja wa klabu hiyo, Marco Silva ilisababisha aachane na uhamisho huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports, Watford itafikiria juu ya kumruhusu nyota huyo aondoke kama ofa ya walau pauni milioni 40 itapelekwa mezani
Everton itazikabili Manchester United na Chelsea kumsajili straika huyu Everton itazikabili Manchester United na Chelsea kumsajili straika huyu Reviewed by Zero Degree on 4/10/2018 05:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.