Loading...

'Power Bank' yazua taharuki Bungeni


Bunge limetoa ufafanuzi kuhusu moshi uliotanda na kuzua taharuki jana bungeni na kusababisha bunge kuahirishwa kabla ya muda wake.

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema chanzo ni ‘power bank’ iliyokuwa ikichaji simu mbili kwa wakati mmoja kwenye droo ya meza ya Mbunge Nsimbo, Richard Mbogo.

Dk. Tulia amesema tukio hilo lilitokea saa 1:20 usiku wakati kikao cha bunge kikiendelea ambapo ulitokea mlipuko wa kifaa cha kielektroniki cha kuchajia simu ya mkononi (power bank) na kusababisha harufu kali iliyotanda kutanda moshi katika ukumbi wa bunge hasa upande wa kulia wa kiti cha Spika.

“Kwa mujibu wa maelezo ya askari wa Bunge mlipuko ulitokea kwenye power bank ambayo ilikuwa ikichaji simu mbili kwa wakati mmoja kwenye droo ya meza ya Mheshimiwa Mbogo ambapo kifaa hicho kiliteketea kwa moto, kuanguka chini na kuunguza zuria na pembeni mwa kiti cha mbunge huyo.

“Katika tukio hilo hakukuwa na majeruhi isipokuwa baadhi ya wabunge walipata mshtuko na baadhi yao walikimbia nje ya ukumbi wa bunge na waliobaki ndani ya ukumbi walipaliwa na moshi na kuanza kukohoa,” amesema.
'Power Bank' yazua taharuki Bungeni 'Power Bank' yazua taharuki Bungeni Reviewed by Zero Degree on 4/10/2018 05:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.